Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega.
Na Mwandishi Wetu.
OFISI
ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeanza kukagua
taasisi za umma kuhusu utekelezaji wa matakwa ya sheria inayowataka
kuwatambua waajiriwa walionufaika na mikopo ya elimu ya juu na
kuwasilisha makato kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB).
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega, sheria
iliyoanzisha HESLB inazitaka taasisi zzote za umma kuijulisha Bodi kwa
maandishi kuhusu waajiriwa wapya katika taasisi hizo ndani ya siku 28 na
Bodi kuthibitisha kama waajiriwa hao ni wanufaika wa mikopo au hapana.
“Baada
ya kuajiriwa mtu huyo ambaye amepata elimu yake ya chuo kikuu au
taasisi yoyote ya elimu ya juu nadni au nje ya nchi kuanzia mwaka 1994
hadi sasa, mwajiri anapaswa kuitaarifu Bodi kwa maandishi ndani ya
kipindi cha siku 28 tangu ajira hiyo,” inasomeka sehemu ya taarifa ya
hiyo iliyochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari jana ikiwemo tovuti
ya HESLB.
Taarifa
hiyo, ambayo pia inapatikana katika tovuti ya HESLB, inaongeza kuwa
baada ya Bodi kupokea taarifa kutoka kwa waajiri hao na kuthibitisha
kuwa waajiriwa ni wanufaika wa mikopo, mwajiri atapaswa kuijulisha Bodi
na kuanza kukata sehemu ya mshahara wa mwajiriwa ndani ya siku 30 na
kuwasilisha makato hayo kwa Bodi ndani ya siku 15 kabla ya kila mwisho
wa mwezi.
Kwa
msingi huo, HESLB kupitia tangazo hilo, HESLB imewajulisha waajiri kuwa
CAG amejumuisha matakwa hayop ya kisheria katika kazi zake za ukaguzi
katika taasisi za umma kwa lengo la kuongeza kasi ya ukusanyaji mikopo
iliyoiva.
“Ni
imani ya HESLB kuwa waajiri katika utumishi wa umma watatoa ushirikiano
kwa ofisi ya CAG ili kuondokana na matatizo ya kisheria,” amesema Bw.
Nyatega katika taarifa yake.
HESLB
ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai 2005 ili,
pamoja na mambo mengine, kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa Tanzania
wahitaji na kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika wa mikopo
hiyo tangu mwaka 1994.