MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Jan 14, 2016

Waziri Muhongo :Ahadi ya Jan 15 Iko pale pale

images

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesisitiza kauli yake kwamba tarehe iliyopangwa kati yake na Mameneja wa Tanesco nchi nzima ya kuhakikisha inawaunganishinia umeme wateja waliolipa kwa kipindi kirefu ikiwemo kukamilisha  matatizo ya  LUKU bado iko palepale.
Profesa Muhongo ameyasema hayo  leo wakati wa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na kuongeza kuwa  tarehe 15 Januari,2016, ndio tarehe ya mwisho ya kukamilisha shughuli hizo nchi nzima.

“Katika hili nasema kweli hakuna mzaha. Hatutanii. Wananchi wamechoka, wanataka umeme. Mtindo wa kuandikiana barua tena haupo. Ukishindwa , unajiondoa mwenyewe”,amesisitiza Prof. Muhongo.

Akijibu hoja za Kandoro kuhusu suala la Makaa ya mawe, amesema atahakikisha suala hilo linapata ufumbuzi wa haraka kuhakikisha rasilimali hiyo inatumika kama chanzo kingine cha kuzalisha umeme nchini.

“Mkuu wa Mkoa hili lazima tulishughulikie. Hatuwezi kuacha makaa ya mawe yakae tu kama mapambo wakati tunahitaji sana nishati ya umeme kwa ajili ya kuondoa matatizo ya umeme tuliyonayo”.
Prof. Muhongo ameongeza kuwa, tayari amewaagiza wawekezaji wote wa makaa ya mawe wenye leseni kukutana  nae katika ziara  ili kukubaliana kuhusu suala hilo.” Tayari nimewaambia wote tukutane huku huku site wanieleze wanafanya nini”, ameongeza.