Afisa
uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (katikati), akijaribisha
moja ya mashine mashine walizomkabidhi kijana Fikiri Chinji (kushoto),
anayejishughulisha na ufundi seremala, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa
Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye karakana yake
iliyojengwa na Airtel katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma mwishoni
mwa wiki hii. Anayeshuhudia (kulia) ni Meneja mauzo manispaa ya Dododma
Hendrick Bruno.
Kijana
Fikiri Chinji anayejishughulisha na ufundi seremala, akionyesha jinsi
mashine yake mpya aliyokabidhiwa na Airtel Tanzania, kupitia mpango wa
Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, inavyofanyakazi katika hafla fupi
iliyofanyika kwenye karakana yake iliyojengwa na Airtel katika Mtaa wa
Ng’ong’o na manispaa Dodoma mwishoni mwa wiki hii. Anayeshuhudia ni
Meneja masoko manispaa ya Dodoma Saidimu Ngalesoni (kulia) akifuatiwa
na Meneja mauzo manispaa ya Dodoma, Hendrick Bruno (wa pili kulia)
Afisa
uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa nne kulia),
akimkabidhi kijana Fikiri Chinji (wa tano kushoto), anayejishughulisha
na ufundi seremala, msaada wa vifaa mbali mbali vya ufundi na kujengewa
karakana mpya kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika
hafla fupi iliyofanyika kwenye karakana yake iliyojengwa na Airtel
katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma mwishoni mwa wiki hii.
Wanaoshuhudia ni wanakijiji wa Ng’ong’ona na wafanyakazi wa Airtel
waliofika kushuhudia tukio hilo.
Wanakijiji
wa Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma wakiangalia banda alilokabidhiwa
Kijana Fikiri Chinji (hayupo pichani) anayejishughulisha na ufundi
seremala, pamoja na msaada wa vifaa mbali mbali vya ufundi kupitia
mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, mwishoni mwa wiki hii.