Maombi yalifanyika kwake na mke wake ili Mungu amtangulie katika utumishi wake serikalini .
Apostle Onesmo Ndegi,Mke wake Lilian Ndegi na Mch. Peace Matovu wakifanya maombi kwa Mh. Makonda .
Mhe.Paul Makonda siku ya leo (jana)
alikuwa anatimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Walaya
Kinondoni,asubuhi ya leo katika Ibada Kanisani Living Water Center
Ministry Kawe alipolelewa kiroho na anapo abudu alikuja kumshukuru Mungu
na kutoa sadaka ya shukrani kwa hatua ambayo amefika.
Katika
Ibada hiyo Mh Paul Makonda aliongozana na Mkee wake alipopewa
kuzungumza alisema anamshukuru Mungu kwa kutimiza mwaka tangu ateuliwe
kuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni,alisema haikuwa raisi kwake ila Mungu
amemuwezesha,akaongeza kwa kusema "usishindwe kufanya mambo ya
kimaendeleo kwa changamoto za kimazingira au chochote kama kwake ambavyo
imekuwa ikionekana".
Mapema
akimkaribisha kuzungumza Mhe.Paul Makonda Kiongozi wa Kanisa hilo
Apostle Onesmo Ndegi alikuwa anaelezea jinsi ambavyo amemlea kiroho
Mh.Makonda hata kabla ya kuingia kuwa mtumishi wa serikali jinsi
alivyokuwa mbunifu wa shughuli mbalimbali hivyo kinachofanyika leo sio
kipya kwake.
Baada ya Ibada hiyo ya shukrani Bwana akatenda zaidi kwa kumfanya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
Hongera Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es saam