Na Musa Mateja, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: KUFURU! Mama wa
staa mwenye jina kubwa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura
Kasimu ‘Sandra’ amedaiwa kufanya kufuru ya aina yake kwa kununua mtaa
mzima, Tandale-Uzuri jijini Dar na kuikarabati nyumba yake aliyokuwa
akiishi zamani kwa kutumia takriban shilingi milioni 100.
Diamond na Mama yake Sandra.
Chanzo chetu makini ambacho kilifuatilia ishu nzima tangu nyumba hiyo
ilipoanza kukarabatiwa, kimesema kwamba kwa kipindi kirefu ‘bi mkubwa’
huyo amekuwa akifika nyumbani hapo asubuhi na kuondoka jioni akisimamia
ujenzi sambamba na binti yake, Esma.
Nyumba hiyo kabla ya kukarabatiwa.
“Mama Diamond noma, kateketeza shilingi milioni 100 na bado nasikia
ameshafanya mchakato wa kununua nyumba za jirani ili mtaa mzima uwe
wao,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kimezidi kutiririka kuwa
mama Diamond anataka kuifanya nyumba hiyo kuwa bora zaidi kwani mbali na
kuiboresha, kuna mpango wa kutengenezwa swimming pool (bwana la
kuogelea).
Baada ya kukarabatiwa.
“Jamani!
Taarifa hizi mmezitoa wapi tena? Kweli nimekarabati nyumba yetu iwe
bora zaidi. Hayo mambo ya gharama na mipango mingine ni siri labda mje
mmuulize Diamond akirudi Marekani lakini ukarabati huu mnaouona ndio
nimeusimamia mimi na mwanangu Esma,” alisema mama Diamond.