
Kwa mara ya kwanza, wadau wa Sanaa nchini wamepata fursa ya kukutana
na Makampuni, Mashirika na Vyombo mbalimbali katika mafunzo
yaliyofanyika hotel ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam. Semina hii
iliongozwa na Maria Sarungi Tsehai, ambaye ni mdau mkubwa katika sekta
hii.

Mafunzo hayo yalifanywa na wataalam kutoka sekta mbalimbali kama
Nyumba, Urembo, Saikolojia, Sanaa na Wasanii n.k


Wadau wa Sanaa pia walipata mafuzo ya Namna ya kubalansi maisha yao ya
Sanaa na yale ya Familia, kutoka kwa mwanasaikolojia maarufu, Aunt
Sadaka Gandi.


Semina hii iliyopewa jina Celebrity Corporate Conference &
Cocktail iliwahusisha pia COSOTA na BASATA ambao ni wasimamizi wakuu
wa kazi za sanaa na taratibu zake

Ms Doreen Anthony Sinare, CEO wa COSOTA akitoa somo kuhusu usajili wa
kazi, masharti ya kuzingatiwa na Sheria zinazomlinda Msanii
aliyesajiliwa

Sekta lengwa katika semina hii ni wadau kutoka Filamu, Muziki, Urembo,
Habari, na Wajasiriamali mashughuri