Aliyekuwa Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi enzi za uhai wake.
Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi
amefikwa na umauti jana majira ya saa tatu na nusu usiku katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na ndugu yake, Dk. Makongoro
Mahanga ambaye alieleza kuwa familia ipo katika taratibu za awali za
msiba huo na kwamba leo watatoa taarifa rasmi na taratibu nyingine.
“Taarifa za kifo cha Dk. Masaburi ni za kweli ingawa sijaenda
hospitali, ninafanya mawasiliano na familia lakini taarifa kamili kuhusu
msiba zitakuwa zikitolewa na msemaji wa familia ambaye tutamteua usiku
huu, na kesho (leo) tutaeleza kiundani,” Alisema Dk. Mahanga jana usiku.
Marehemu pia aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Mtandao huu unatoa pole kwa Taifa kwa ujumla kwa msiba huu wa
aliyekuwa kiongozi wa ngazi mbalimbali akiutumikia umma. Apumzike kwa
Amani. Amina!