Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi
Kida (kushoto) akisalimiana na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.
Jenista Mhagama (kulia) alipowasili katika ukumbi wa shule ya msingi
Allience mjini Bariadi kufungua kongamano la vijana.
Mhagama
alisema katika Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Mkoa wa Simiyu,
kuratibiwa na Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) chini ya
ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwamba kuna
fursa nyingi lakini vijana wanakuwa wagumu kuzichangamkia na matokeo
yake kubaki wakiilalamika serikali kuwa haiwajali.
Alibainisha kuwa serikali itaendelea kusaidia makundi ya vijana yanaoonesha nia ya kujiendeleza
Aidha
alifafanua kuwa itawaongezea mtaji wa shilingi milioni 30 kwa kikundi
cha vijana cwalioanzisha kiwanda Maziwa cha Meatu pamoja na kile cha
Chaki kutokana na jitihada zao walizofanya na matunda kuonekana.
Awali
kabla ya kumkaribisha mgeni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka
alisema lengo la serikali mkoani hapa ni kuhakikisha linainua pato la
mkoa na kuchangia katika pato la taifa kwa kuwawezesha vijana wake
kutengeneza bidhaa zinazotokana na malighafi zinazozalishwa mkoani hapa.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Mh. Jenista Mhagama na Naibu wake Mh. Anthony Mavunde
wakisalimiana na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na ESRF mara baada
ya kuwasili kwenye kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika jana
katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Alisema
zaidi kwamba wanalengo la kuhakikisha mkoa unaingia katika tano bora ya
uchangiaji wa pato la taifa.Amehimiza viongozi kuwasaidia vijana
kuwaongoza, kuwaelekeza na amewataka vijana kuwa na uthubutu na kuungana
kwa pamoja.
Pamoja
na harakati za kiuchumi vijana wametakiwa kuwa na mwendo wenye maadili
mema ili kuendelea kuwa na afya bora na kukwepa magonjwa yanatokanayo na
ukosefu wa maadili.Amesistiza kuwa kauli mbiu waliyoanzisha ya “Bidhaa
moja,wilaya moja” itumike ipasavyo ili kufanikisha maendeleo yao na ya
wilaya.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la
vijana Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi
Allience mjini Bariadi.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF),
Dk.Tausi Kida alisema ushiriki wa vijana katika viwanda vidogovidogo
kunaweza kukuza uchumi kutokana na viwanda hivyo kutoa ajira na pia
kutengeneza mnyororo wa thamani katika mazao ya wakulima ambako vijana
ndiko wanakotarajiwa kuonesha ushujaa wao.
Hata
hivyo alisema ukuaji wa uchumi kwa sasa bado ni changamoto kwa wananchi
wanaoishi vijijini kutokana na baadhi ya huduma kutowafikia kwani
asilimia 7 inayopanda kiuchumi huwa haitafsiriki kufikia makundi yote ya
kijamii .
“Tumekuwa
tukiendesha tafiti nyingi lakini tunaona kipato chetu kinaendelea
kushuka hasa katika wananchi wanaoishi vijijini hivyo kuwepo kwa viwanda
kutaweza kuwainua kiuchumi wananchi kutokana na bidhaa zao ghafi kuuzwa
katika viwanda”Alisema Dk. Kida.
Nao wafadhili wa Kongamano hilo UNDP wamesema wametenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia vijana katika programu zao za maendeleo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Waziri Mhagama.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza machache awali kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama
kufungua kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika jana katika ukumbi
wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Waziri
wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico akitoa salamu kwa vijana kutoka
visiwani Zanzibari kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika
jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Meza
kuu mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, Waziri wa Kazi,
Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Mhe. Moudline Castico (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu Dk.Titus Kamani ( wa pili kulia), Mkuu wa Programu, Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama (kulia), Mkurugenzi
Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida (kushoto), Naibu Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh.
Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Anthony Mtaka (wa tatu kushoto).
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya kuondoa Umaskini wa Wizara ya Fedha na Mpiango,
Mudith Cheyo (kulia) na Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya
Fedha na Mipango, Maduka Kessy wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa
kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule
ya msingi Allience mjini Bariadi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida akiwasilisha mada ya mageuzi ya
kiuchumi yanayohitajika kuboresha maisha ya vijana pamoja na hali ya
uchumi nchini kwa makundi ya vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini
walioshiriki kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika
ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Bw.
Abdallah Hassan (kushoto) na John Kajiba wa ESRF wakifuatilia jambo
kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa
shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Mkuu
wa Programu, Shirika la Maendeleo UNDP, Amon Manyama akizungumzia
mchango wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN/UNDP) katika Maendeleo
Endelevu ya Vijana wakati wa kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika
jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Sehemu
ya umati wa vijana na wageni waalikwa waliohudhuria kongamano la vijana
Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience
mjini Bariadi.
Naibu
Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka
Kessy akiwasilisha mada ya fursa za vijana katika uchumi wa viwanda
pamoja na Mpango wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano 2016/17-2020/21
kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa
shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Mkurugenzi
wa Mafunzo ya Ufundi Stadi-VETA Leah Dotto akiwasilisha mada
iliyozungumzia mchango wa elimu ya ufundi stadi katika kufikia Tanzania
ya viwanda katika kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika
ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Afisa
Mwandamizi wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Abdallah Hassan
akizungumzia fursa mpya ya kilimo biashara kwenye kongamano la vijana
Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience
mjini Bariadi.
Pichani
juu na chini washiriki wakiuliza maswali kwa wakufunzi na viongozi wa
serikali katika kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika
ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Pichani
juu na chini ni umati wa makundi ya vijana kutoka maeneo mbalimbali
nchini ikiwemo Vyuo Vikuu waliohudhuria kongamano la vijana Simiyu,
lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini
Bariadi.
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama na Naibu wake, Mh. Anthony
Mavunde katika picha ya pamoja na mdhamini mkuu wa kongamano hilo UNDP,
waratibu ESRF pamoja na wawasilishaji mada kwenye kongamano la vijana
Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience
mjini Bariadi.
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Anthony Mtaka katika picha ya pamoja na wawasilishaji mada, ESRF pamoja
na UNDP kwenye mabango ya viwanda vilivyoanzishwa na vijana cha Meatu
Milk na kiwanda cha kwanza Tanzania cha kutengeneza Chaki cha mkoani
Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Anthony
Mavunde wakimtunza mwanakikundi wa ngoma za asili cha Wanaisanga kutoka
Maswa mwenye uzoefu wa kucheza na Chatu wakati wa burudani kwenye
kongamano la vijana Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya
msingi Allience mjini Bariadi.
Mwanakikundi
wa ngoma za asili Wanaisanga kutoka Maswa mwenye uzoefu wa kucheza na
Chatu akionyesha umahiri wake wa kucheza na chatu kwenye kongamano la
vijana Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi
Allience mjini Bariadi.
Kutoka
kulia ni Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na
Mipango, Maduka Kessy, Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama, Mtafiti Mshiriki ESRF, Dr. Oswald
Mashindano, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dr. Tausi Kida, Mkuu wa Idara
ya Maarifa na Ubunifu ESRF, Margareth Nzuki wakifurahi burudani ya ngoma
za asili ya kucheza na Chatu wakati wa kongamano la vijana Simiyu,
lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini
Bariadi.
Wageni waalikwa wakiendelea kufurahi burudani ya ngoma za asili kwenye kongamano la vijana Simiyu.
Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika kongamano la vijana Simiyu waliwakilisha.
TABIA ya vijana kutojishughulisha katika miradi mbalimbali yenye tija kumeeelezwa kuwa moja ya vyanzo vya kudorora kwa uchumi.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama katika ufunguzi wa
kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika katika ukumbi wa shule ya
msingi Allience Mjini Bariadi.
Alisema
kumeanza kujitokeza hali ambapo vijana nchini kutokupenda
kujishughulisha katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na hivyo kushindwa
kuondokana na umaskini na pia kuchangia katika pato la taifa.
Alisema
kuwa vijana wanaongoza kwa idadi kubwa lakini wanashindwa
kujishughulisha kuhakikisha wanapata maendeleo ambayo yanaweza
kulisaidia taifa.