Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
inautaarifu umma kuwa imesitisha mikopo ya elimu ya juu iliyokuwa
ikitolewa kwa walimu-wanafunzi wanne waliosimamishwa masomo kwa kuhusika
katika tukio la kumshambulia na kumuumiza mwanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Kutwa ya Mbeya. Walimu hao walikuwa katika mafunzo ya
vitendo.
1. Frank Msigwa – Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
2. John Deo- Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
3. Evance Sanga – Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
4. Sante Gwamaka – Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)
Kwa utovu huo wa nidhamu, wanafunzi hao wamesimamishwa masomo na
mamlaka husika kwa hiyo wamepoteza sifa za kuendelea kupokea mikopo.
Mikataba inayosainiwa na wanufaika wa mikopo inawataka wanufaika
kuzingatia masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na nidhamu na kufuata sheria
na taratibu za vyuo na mamlaka halali.
Aidha, kwa mujibu wa taratibu za kukopeshwa, wanafunzi hawa watatakiwa kuanza kurejesha kiasi walichokopeshwa mara moja.
Bodi ya Mikopo inawakumbusha wanufaika wanaoendelea masomo
kuzingatia masharti ya ukopeshwaji na kuheshimu sheria, kanuni taratibu
na kuwa mfano mwema katika jamii. Mikopo na ruzuku zinazotolewa na
Serikali ni kwa ajili ya kuwaandaa kuwa raia wema, waadilifu, na wachapa
kazi ili kujenga uchumi imara na ustawi kwa wote.
Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji
Ijumaa, Oktoba 7, 2016