Kiongozi wa upinzani Gabon, Jean
Ping, ametaka watu wasishirikiane na Ali Bongo kama kiongozi wa taifa
baada ya uchaguzi wa Agosti uliokumbwa na mzozo.
Kiongozi aliyepo sasa Bongo, alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo, lakini Ping anasisitiza kuwa yeye ndiye aliyeshinda.Upinzani unasema watu kadhaa waliuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi.
Jean Ping ametia saini taarifa yake kama 'rais mteule' - wadhifa usiotambuliwa, na tume ya uchaguzi nchini.
Kiongozi huyo wa upinzani ameshutumu alichokitaja kuwa mapinduzi ya kijeshi katika uchaguzi dhidi yake.
Anataka raia wote wa Gabon wanaompinga rais Ali Bongo wajumuike na kushirikiana katika kumtenga kimataifa.
Bwana Ping ametaka pia Bongo aidhinishiwe vikwazo na viongozi wengine kadhaa akiwemo mkuu wa mahakama ya katiba iliyopinga malalmiko aliyowasilisha kupinga uchaguzi huo.
Lakini hatakama kuna wasiwasi wa kimataifa kuhusu uchaguzi huo, Rais Bongo haonekani kuwachia madaraka wakati wowote hivi karibuni.
chanzo:bbc