Maafisa katika jimbo la Kaduna
Nigeria wameharamisha vuguvugu la kiislamu Nigeria - Islamic Movement of
Nigeria - kundi kuu la madhehebu ya shia nchini humo.
Kwa kunukuu
sheria kadhaa - serikali ya jimbo hilo imesema uamuzi wa kulipiga
marufuku kundi hilo ni katika kuhakikisha amani na usalama katika jimbo
hilo la kaskazini magharibi.Serikali inasema tangu kuzuka ghasia kat iya jeshi na kundi hilo la kiislamu mnamo Desemba mwaka jaba - wafuasi wa kundi hilo wameendelea kuvunja sheria.
Jambo ambalo maafisa wa serikali katika eneo hilo wanasema hawawezi kulipuuza.
Kwa amri hii, msemamji wa serikali hiyo ameongeza kuwa kuanzia sasa mtu yoyote anayejihusisha au akatekeleza mambo kwa jina la kundi hilo atashtakiwa Makao makuu a kundi hilo ni mji wa Zaria kaskaizni magharibi mwa jimbo la Kaduna.
Inaslia kuonekana ni vipi amri hii itaathiri matawi mengine ya kundi hilo nchini.
Tume ya mahakama ilipendekeza kushatakiwa wote waliohusika katika mapigano kati ya jeshi na madhehebu ya Shia ambapo jeshi lilituhumiwa kwa kuawaia wafuasi 347 wa kundi hilo.
Mpaka sasa hakuna aliyeshtakiwa.
Mwanajeshi mmoja pia aliauwa katika ghasia hizo.