MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Oct 8, 2016

Watu 800 wafariki Haiti baada ya kimbunga Matthew

Umoja wa mataifa umeonya kuwa huenda ikachukua siku kadhaa kwa athari kamili ya kimbunga Matthew kujulikana nchini Haiti wakati idadi ya waliokufa imeongezeka hadi 800.
Idadi hiyo imezidi mara mbili wakati maafisa wa uokozi wanafika katika maenoe ya kusini ambaye imekuwa vigumu kuyafikia kutokana na mvua kali.
Carlos Veloso wa Shirika la chakula duniani anasema miji iliyoathirika zaidi yanayweza kufikiwa kwa njia ya anga au majini pekee.
Vifo vingi Haiti vimetokea kusini magharibi mwa pwani ya eneo hilo, lililoathirika pakubwa na kimbunga hicho wiki iliyopita.
Kimbunga Matthew kimetua pwai mwa jimbo la Florida Marekani lakini kimepungua kasi na kuwa cha kiwango cha pili kikiwa na upepo wenye kasi ya kilomia 177 kwa saa.
Kimbunga cha kiwango cha tano ndicho kikali zaidi katika mizani ya Saffir-Simpson ya uzito wa vimbunga.
Jitihada za kutafuta manusura zinaendelea kufutia kimbunga hicho kilicho kibaya kuwahi kushuhudiwa katika visiwa vya Caribbean katika muda wa muongo mmoja.
Shirika la ulinzi wa raia Haiti Ijumaa limesema idadi ya waliofariki imeongezeka mara mbili zaidi kutoka watu 400 hadi watu 800.
Maafisa wa uokozi wanasema wanatarajia kupata waathiriwa zaidi wanapokaribia maeneo ya mashinani.
Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la watoto katika mji wa Port-Au-Prince, Cornelia Walther, ameiambia BBC kwamba, kupatikana maji safi ni muhimu zaidi kwa sasa.