Maafisa wa polisi nchini Kenya
wamewakamata watu 40 wa jamii ya Oromo kwa kufanya maandamano kinyume na
sheria katika mji mkuu wa Nairobi,kulingana na gazeti la Daily
Nation.
Gazeti hilo limemnukuu afisia mkuu wa polisi wa eneo la
Gigiri Vitalis Otieno akisema kuwa maafisa wa polisi waliitwa katika
eneo hilo baada ya kundi hilo kuzua ghasia.''Wengine wao wako nchini kinyume na sheria...tunawachunguza na kukagua nakala zao'',aliongezea.
Kiongozi wa kundi hilo hatahivyo amesema kuwa waliwaelezea maafisa wa kaunti kuhusu mkutano huo mnamo tarehe 29 mwezi Septemba ,2016 na kulipa fedha zinazohitaji za shilingi 3000 kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Mkutano huo unafuatia ripoti za watu kutoka kwa jamii ya Oromo ambao inadaiwa kuwa waliuawa katika mkanyagano wakati wa maandamano siku ya Jumapili nchini Ethiopia.