Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto),
akiangalia taarifa zinazoingia katika mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu
alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo mahiri cha kuhifadhi
Kumbukumbu cha Taifa (Internet Data Centre), kilichopo eneo la
Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Msimamizi
wa masuala ya TEHAMA Bw. John Chorai (kulia), akimuonesha Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), namna
kifaa cha kurekodia malipo kinavyofanya kazi wakati alipofanya ziara ya
kushtukiza katika Kituo mahiri cha kuhifadhi Kumbukumbu cha Taifa
(Internet Data Centre), kilichopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia), akikagua moja ya kifaa cha kuhifadhi Kumbukumbu katika kituo
Mahiri cha Internet Data Centre cha Taifa kilichopo eneo la Kijitonyama
jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza
kushoto), akifafanua jambo kwa watumishi wa kituo Mahiri cha kuhifadhi
Kumbukumbu cha Taifa (Internet Data Centre), kilichopo eneo la
Kijitonyama jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza
kituoni hapo.
Mwakilishi
wa Kibiashara kutoka Ubalozi wa Uingereza anayesimamia nchi ya Tanzania
na Kenya Bw. Lord Hollick (wa pili kulia) akifafanua jambo kwa Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza
kulia) wakati alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia masuala ya
kuboresha miundombinu nchini. Kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini Bi
Sarah Cookie.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano