![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWUlLaVlhj82WW-kNEaRUg1KkoIuVTuXPD0sEsJTiVffYuOxGGuUfwK5t2hcWG1DUNN-UEVrUugmyToYWYAY1tADzWROGenIJYWUs7uthgsekAxJx0UJaDc7q359SfOlJ7sKTtYgk-FDQ/s640/WhatsApp+Image+2016-11-25+at+17.40.57.jpeg)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amempongeza mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda kwa juhudi anazofanya katika
ziara yake kwa kusikiliza kero za Wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.
Rais
Magufuli ambaye alimpigia mkuu huyo wa mkoa wakati alipokuwa akisikiliza
kero za Wananchi katika Kata ya Mbezi Luis eneo la Malamba Mawili
ambako aliweza kumsisitiza kuwa aendelee kutumbua watu huko huko aliko.
“Endelea
hivyo kutembelea wananchi na kutoa ufafanuzi kwa sababu nyingine
ufafanuzi huu kama ungetolewa mapema wala wananchi wasingekuwa na sababu
ya kuja kuuliza maswali kui kwa hiyo endeleeni hivyo hivyo na juhudi za
Dar es Salaam na wakuu wa Wilaya yako na watendaji wote kwa kazi nzuri
mnazozifanya kwa kusikiliza kero zao bila kujali vyama vyao bila kujali
makabila yao na uendelee kutumbua huko huko” Amesema Rais Magufuli.
Amemtaka
pia kuendelea kupiga kazi na kumwabia kuwa yeye yupo nyuma yake kwani
amevunja mwiko wa viongozi waliokuwa wanapendelea kukaa ndani. Kwa
upande wake mkuu huyo wa mkoa aliendelea kuwa mtiifu huku akimsikiliza
Rais Magufuli kwa Makini juu ya pongezi anazopewa mbele ya watu kwani
ameweza kurudisha imani kwa viongozi wa serikali ambayo iliondoka kwa
watu kutokana na ujinga wa watu wa chache. Mhe. Makonda.