Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) na kumteua Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho.Rais Magufuli
Awali
nafasi hiyo ilikuwa chini ya Bi. Juliet Kairuki ambaye alitenguliwa na
Rais Magufuli 24 Aprili mwaka huu baada ya Rais kupata taarifa kuwa
kiongozi huyo alikuwa hachukui mshahara wa serikali tangu alipoajiriwa
mwaka 2013.