Malkia wa filamu bongo, Wema Issac Sepetu amefunguka na kuwataka
mashabiki wamuombee apate mume bora atakayekuwa na heshima na wala
asiwe mtu maarufu na siyo kumhusisha kila mara na uhusiano wa kimapenzi
na msanii Diamond Platnumz. Wema
amefunguka hayo wakati akimjibu Shabiki katika kurasa wake wa
Instagram, na kumtaka atambue Diamond ni baba wa watoto wa wili kwa sasa
na ifike kipindi watu wanatakiwa wakubali kuwa hakuna kinachoendelea
kati yake yeye na Diamond bali wamuombee na yeye apate mume wake ambaye
siyo mtu maarufu.
"Sasa baby aliokwambia
namtaka Damond ni nani? Life has to go on, yule ni baba wa watoto wawili
jamani. Its about time u guys accept that Me and Naseeb no more.
Mnachotakiwa kuniombea ni nipate mwanaume bora na siyo bora mwanaume na
mwenye heshima zake"- aliandika Wema Sepetu.
Koment ya Wema akimjibu shabiki aliyandika kuhusu wema kumtaka Diamond.