Hiyo
ni fedha ambayo Dawasco wanadaiwa na bodi hiyo ikiwa ni malimbikizo ya
makato ya wadaiwa ambao Dawasco imewakata lakini imeshindwa
kuyawasilisha katika bodi hiyo
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji
Madeni kutoka Bodi ya Mikopo amesema Dawasco wametenda kosa kisheria
kushindwa kuwasilisha fedha hizo licha ya kuwa wamekwishawakata
waajiriwa wanaodaiwa na bodi hiyo.
Pia ametoa onyo kwa waajiriwa wa
mashirika, taasisi, na makampuni mbalimbali kuhakikisha kuwa
wanawasilisha fedha hizo kwa wakati bila kufuatiliwa na bodi.
Tangu kufanyika kwa mabadiliko ya
kisheria ya kiwango cha makato kutoka asilimia 8 hadi asilimia 15, bodi
ya mikopo imeweza kukusanya shilingi bilioni 12 kwa mwezi mmoja pekee
kutoka kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa mwezi kabla ya kubadilika kwa
kiwango hicho cha makato.