Dkt. Hamis Kigwangalla na Francis Maige Ngosha ambaye ni mmoja wa wachora nembo ya taifa, alipomtembelea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Serikali ya imelazimika
kumuhamishia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mzee Francis Maige
Ngosha aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Amana kwa kipindi cha siku
moja kwaajili yakupatiwa matibabu zaidi. Akitoa
tamko la serikali Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Khamisi Kigwangalla amesema mzee huyo ambaye ni
mmoja wa wachora Nembo ya Taifa amesema wameamua kumuhamishia katika
hospital hiyo ya Taifa Muhimbili ili kufanyiwa uchunguzi wa kina na
wataalamu wa magonjwa mbalimbali ili kubaini na kutibiwa.
Dkt. Kigwangalla amesema serikali
itahakikisha inampa tiba kamili na malezi kwa kuzingatia haki ya kuishi
ya binadamu na kuthamini mchango wa wazee na waasisi wa taifa.
Kwa upande wake daktari bingwa wa
magonjwa ya dharura kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma
Mfinanga amesema wanasubiri majibu ya vipimo wanavyomchunguza na pindi
watakapobaini tatizo atapatiwa matibabu yake.
Kwa upande wake Francis Maige Ngosha
ambaye ni mmoja wa wachora Nembo ya Taifa ameishukuru serikali na jami
iliyokuwa ikimlea kwa miaka yote bila malipo.
Nembo ya Taifa