Stanslaus Mabula (Kulia), Rais Magufuli (kushoto)
Mbunge wa jimbo la Nyamagana
Stanslaus Mabula amefunguka na kuwataka Watanzania kumshukuru sana Rais
wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na maamuzi yake
aliyofanya jana kuhusiana na sakata la usafirishaji wa mchanga na
madini.
Mabula
amesema Rais Magufuli anastahili kupongezwa na kila Mtanzania kwa jambo
hilo kwani miaka mingi serikali imekuwa ikipoteza mapato na kupata
hasara kutokana na mambo haya.
"Makontena haya zaidi ya
miambili mpaka miatatu kusafirishwa nje yaani hapo serikali imepata
hasara kubwa sana, unajua mimi ni Mjumbe wa Kamati ya PAC na mara kadhaa
wamekuwa wakiomba mikataba ya madini ikaguliwe sasa haya ndiyo matokeo
Mh. Rais alitambua na alizungumza sana kwenye kampeni yake kabla
hajafika kwenye masuala ya kuangalia mikataba uchunguzi unajibiwa kwa
uchunguzi. Kwa hiyo uchnguzi huu ni sahihi kwenda kufumua mikataba na
kuona wapi tulipoanguka na wapi tunataka kwenda kwa ajili ya maisha ya
Watanzania" alisistiza Mabula
Mabula aliendelea kufafanua kuwa
"Ukifanya mahesabu ya haraka
haraka ambazo wataalamu wa hesabu wamekuwa wakizungumza baada ya Rais
Magufuli kufanya maamuzi jana inaonekana karibia nusu ya bajeti ya
serikali kwa mwaka mzima inapotea, sasa unaweza kuona kiasi gani cha
fedha hizi zimekuwa zikipotea na sasa hivi tunafikiria kutumia tilioni
31 lakini karibia tilioni tisa tunataka kuzipata kutoka kwa wahisani
kumbe tilioni tisa zinapotea kwenye mikono yetu, kwa hiyo yote haya
inaonyesha jinsi gani Rais wetu anataka kutupeleka sehemu nzuri" alisisitiza Mabula