Rais Uhuru Kenyatta (kushoto)
Tume ya Uchaguzi na Mipaka
nchini Kenya, IEBC, imeidhinisha majina ya wagombea nane kuwania Urais
katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu
Kati
ya wagombea hao, ushindani mkubwa unatarajiwa kuwa kati ya Rais Uhuru
Kenyatta anayewania muhula wa pili na mgombea wa muungano wa vyama vya
upinzani NASA Raila Odinga.
Hata hivyo, zoezi la mchujo liliwaacha
wengine zaidi ya 10 nje ya kinya'nga'nyiro hicho akiwemo Peter Solomon
Gichira aliyefikishwa Mahakamani kwa madai ya kutaka kujiua baada ya
kuondolewa katika orodha hiyo kwa kutokidhi vigezo.
Ushindani unaotarajiwa kati ya Rais
Kenyatta na Bw. Odinga, unarejesha nchi hiyo katika historia ya siasa
kati ya baba zao, Jomo Kenyatta aliyekuwa Rais wa kwanza na Jaramogi
Oginga Odinga aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais baada ya Uhuru mwaka
1963.
Wagombea wengine sita ambao wanawania
Urais ni pamoja na Cyrus Jirongo (UDP), Ekuru Aukot kutoka chama cha
Thirdway Alliance, Abduba Dida (ARC).
Wagombea binafsi ni pamoja na Joseph
Nyagah, Michael Wainaina na Japheth Kavinga, ambao wamejinadi kama
chaguo sahihi la kuleta mabadiliko.