Muft wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubery
Waumini wa dini ya kiislamu
nchini wametakiwa kuutumia vizuri mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kufanya
matendo mema pamoja na kudumisha amani ndani ya taifa la Tanzania
Wito huo umetolewa na Mufti wa Tanzania,
Sheikh Abubakary Zubeiry Ally wakati akizungumza na Hotmix ya EATV
kuhusu kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na kusema kuwa
katika kipindi hiki waislamu wanapaswa kuwasaidia watu wasiokuwa na
uwezo wakiwemo, yatima na watu wengine.
“Nchi ikikosa amani hata
shughuli nyingine za maendeleo na ibada haziwezi kufanyika kama
inavyopaswa, hivyo basi ni muhimu kwa waislamu nchini kuwa mfano wa
kudumisha amani na upendo”. Alisema Mufti
Sheikh Zubery, ameongeza kuwa katika
mwezi huo Mtukufu wa Ramadhan Waislamu wanatakiwa kuishi kwa mapenzi na
upendo, ikiwa ni pamoja kuwangalia na kuwasaidia wale wasiokuwa na uwezo
wakiwemo, mayatima na watu wengine wasiojiweza.
Katika hatua nyingine naye, Sheikh wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum amewasihi waislamu kiujumla
kuutumia mwezi mtukufu wa Ramadhan katika kuiombea nchi pamoja na
kusameheana kwa waliokoseana bila ya kusahau kutoa misaada kwa watu
wasiojiweza.