Klabu ya Yanga SC
imewapongeza wachezaji wake Saimoni Msuva na Haruna Niyonzima kwa
kuondoka na tuzo katika hafla ya ugawaji tuzo za Ligi kuu Tanzania Bara
katika msimu uliomalizika wa 2016/17.
Hayo
yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Idara ya habari na mawasiliano
ya klabu hiyo kwa kusema wanajivunia wachezaji hao kupata tuzo hizo
kwani mafanikio ni chachu katika kuendelea kufanya vizuri katika
mashindano yao kiujumla.
"Uongozi wa klabu ya Yanga
SC pamoja na benchi la ufundi unatoa pongezi za dhati kwa wachezaji wetu
Saimoni Msuva aliyeibuka mfungaji bora wa ligi kuu pamoja na Haruna
Niyonzima aliyenyakua tuzo ya mchezaji bora wa kigeni ....Mafanikio yenu
ndio chachu ya mafanikio ya klabu yetu....Tunajivunia hilo sambamba na
wenzenu wote kwenye kikosi kwa kujituma kwa moyo wote kuhakikisha timu
yenu inakuwa mabingwa wa ligi kuu mara tatu mfululizo". Ilisema taarifa hiyo
Niyonzima ameshinda tuzo hiyo baada ya
kuwashinda Method Mwanjale kutoka Simba na Yusuph Ndikumana wa Mbao FC
huku Saimon Msuva akiwa sawa na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting baada
ya kuwa na idadi sawa ya magoli msimu huo.