Tundu Lissu
Mbunge wa Singida Mashariki
(CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya
kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na
kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.
Tundu
Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo
ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye
mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu
ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu
"Sisi Tanzania ni wanachama
wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee
Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao
kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii
utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko,
tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka
wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa
makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi
tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu
Makontena ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini
Tundu Lissu anasema hili suala
tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja
muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika
katika uchunguzi huo.
"Rais anajiingiza kwenye
mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini
siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray
Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu
alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo
mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu
Rais Magufuli akipokea ripoti ya kamati
Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...
"Kama unataka kufanya haya
unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni
kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama
utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji
wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule
unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi
wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa
watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na
sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza
mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa
hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani
sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu