Wolper na baadhi ya Wasanii wakati wa kampeni za Uchaguzi mkuu 2015.Malkia wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amefunguka sababu za kuacha kuendelea kuisapoti CHADEMA ni viongozi wa chama hicho kushindwa kuutambua mchango wake alioutoa wakati wa uchaguzi mkuu hali iliyomfanya ajihihisi mpweke na kama ametelekezwa
Ikiwa
ni mara ya kwanza Wolper kufunguka ishu hiyo katika kipindi cha
KIKAANGONI kinachorushwa kwenye ukurasa wa facebook EATV,
amesema hajawai kuwa msaliti kwani hakuwa mwanachama wa chama hicho
lakini alisikitishwa na uongozi wa chama kushindwa hata kumshukuru kwa
kazi aliyoifanya wakati wa uchaguzi mkuu kwa kujitoa pasipo kulipwa hata
shilingi elfu 10 za kitanzania.
Pamoja na kuwa alifanya kampeni za
kumsapoti Mgombea uraisi kupitia mwamvuli wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa,
Wolper amedai kuwa hakuwa anasapoti chama kizima bali mgombea kwa kuwa
yeye ni shabiki wa kiongozi huyo na familia yake kwa ujumla ndiyo maana
hakukubali kulipwa katika kampeni hizo.
Wolper akiwa Kikaangoni
"Mimi
nilifanya siasa kwa sababu namkubali Lowassa, na mimi ni shabiki wake na
familia yake kwa ujumla. Nilianza kumsapoti Lowassa tangu yupo CCM.
Mimi ni mfanyabiashara na muigizaji, sijawahi kuwa mwanasiasa ndio maana
nilikuwa namsapoti mtu mmoja mmoja na siyo chama. Hata hivyo mimi siyo
Yuda kwa CHADEMA kwa sababu sijawahi kuwa mwanachama wao na sina chama
chochote lakini wao baada ya uchaguzi walinitelekeza kiasi cha
kunifanya nijisikie mpweke. Hata kama hawakushinda uchaguzi walipaswa
hata viongozi wawili wanishukuru tu kwa maneno ili na mimi nipate faraja
lakini hawakuweza kufanya hivyo.
Hata hivyo Wolper amekiri wazi hata
tatizo na Mhe Lowassa na hawezi kuml;aumu kwa yaliyotokea bali atakuwa
naye bega kqwa bega tena kumsapoti endapo atapata tena nafasi ya
kugombea urais 2020.
Mtazame hapa chini Wolper akifunguka kwa undani zaidi.