RAPA kipenzi cha Watanzania, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ amefunguka
kuwa afya yake imeimarika na sasa yupo tayari kupanda jukwaani kukamua
shoo kama kawaia yake.
ROMA ameyasema hayo jana wakati akitoa neno la shukrani kwa uongozi na
wafanyakazi wa Kampuni ya Glopbal Publishers kwa kuendelea kumsapoti,
kufanya naye kazi, kuboresha mahusiano yaliyo mema na kumfariji hasa
katika kipindi kigumu alipopatwa matatizo ya kutekwa akiwa na wenzake
watatu.
“Nimfika hapa kwa ajili ya kutoa neno la shukrani kwa jinsi ambavyo
tmekuwa tukifanya kazi pamoja, pamoja na matatizo yaliyotukuta mimi na
wenzangu lakini nyinyi Global Publishers mmeendelea kuwa na mimi katika
kipindi chote hicho.
“Mtu akiona nimeweza kutembea kutoka nyumbani mpaka kufika hapa ofisini
(Global PUblishers), basi ajue nipo fiti, na ninaendelea vizuri. kama
nimeweza kushika maiki, nikazungumza basi hata Dar Live naweza kushika
maiki (akimaanisha kufanya shoo).
“Niliona kipindi cha matatizo mlitupigania, magazeti ya Global
Publishers yalifanya coverage nzuri na mlikuwa upande wetu. Kiukweli
tulifarijika kuona watu wengi wakitutia moyo na kutupatia neno la
faraja,” alisema Roma.