
Baada ya kurudi kwenye tasnia ya muziki kupitia wasanii waliotumia
vionjo vya nyimbo zake na hivyo kupelekea watu kumkumbuka tena nguli
huyu, na yeye ameamua kuingia studio kukumbushia makali yake ya kipindi
cha nyuma
Saida Karoli ambaye amekuwa akiimba nyimbo za asili alitamba sana miaka
ya mwanzoni mwa 2000 ambapo waimbo wake ambao ni maarufu zaidi ni
Chambua ambao siku za hivi karibuni wasanii kama Darassa, Belle 9,
Diamond Platnumz walitumia vionjo vya wimbo huo na kutengeneza nyimbo
zao zilizofanya vizuri sana.
Said Karoli ametoa wimbo wake mpya ambao na yeye ametia vionjo vya
wasanii hao waliotumia wimbo wake. Wimbo huo una jina asili ambalo kwa
kiswahili linamaanisha Maneno Maneno. Usikilize wimbo huo hapa chini;