Kuna taarifa kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wamekata rufaa kupinga
adhabu waliyopewa Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya (CHADEMA).
Wabunge hao wamefungiwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa kipindi cha miezi
kumi. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Toleo la 2013, Wabunge hao
watapokea nusu mshahara na nusu posho kwa kipindi chote cha adhabu yao.
Rufaa hiyo, kama ipo kweli, ni hopeless, kupoteza muda na haitafanikiwa.
Kuna sababu mbili za kisheria na kiuhalisia. Kwanza, Kanuni za Bunge
hazina neno 'rufaa' au 'rufani'. Yaani, hakuna suala la rufaa kwa jambo
lolote linaloamuliwa na Bunge (niko tayari kurekebishwa). Katika adhabu
zinazotolewa na Bunge, kwa mujibu wa Kanuni ya 74 ya Kanuni za Bunge,
hakuna rufaa inayozungumziwa.
Kukosekana kwa kifungu maalum katika Kanuni za Bunge kinachohusu rufaa
dhidi ya adhabu kwa Wabunge ni pengo kubwa kisheria katika kuwasilishwa,
kusikilizwa na kuamuliwa kwa rufaa hiyo inayosemwa kuwasilishwa. Bunge,
au Mamlaka iliyopelekewa rufaa, haliwezi kuwa 'moved' kuifanyia kazi
rufaa hiyo kwakuwa hakuna kifungu kinachoruhusu hilo.
Kiuhalisia, Mamlaka zote za Kibunge yaani Spika, Naibu Spika na
Wenyeviti wa Bunge walishiriki katika mchakato mzima wa kufikia uamuzi
huo dhidi ya akina Mdee. Ndiyo kusema, mamlaka zote za Kibunge haziko
'huru' kupokea na kusikiliza rufaa hiyo na kuitolea uamuzi wa haki. La
nyongeza ni kuwa wote wanatoka chama kimoja-chama tawala.
Katika hali kama hiyo, it is advisable to resort to judicial review as
opined by Hon. Tundu Lissu if deemed necessary. Kwa Bungeni, mambo hayo
yalishaisha.
Credit - Petro E. Mselewa ,JF