Sep 24, 2014
Adam Juma ampongeza Izzo Bizness kwa kutaja gharama halisi aliyotumia kwenye video ya ‘Walala hoi’, M 1.4
Director Adam Juma wa kampuni ya Visual lab/Next Level, amempongeza rapper wa Mbeya Izzo Bizness na director wake Nick Dizzo kwa kutaja gharama halisi waliyotumia kushoot video ya ‘Walala hoi’ ambayo Izzo amesema ni shilingi milioni 1 na laki 4 tu.
“Video ni milioni 1 na
laki 4 na Nick hapo tumemlipa kila kitu” Izzo aliiambia E-Newz ya EATV.
Adam kupitia Instagram ameandika:
adamjumanxl–“Nice @Izzo_bizness kwa ukweli wako mzee, I hope wote wawili mnaheshimiana nick dizo na izzo that’s how people work. It doesn’t help wasanii na madirector mkidanganya bei za kazi zenu, tufanya industry islow down tu. Wasanii chipukizi wanaogopa hata kufanya kazi kisa kasikia video mil25 au mil50, creativity sometime inaweza ikacost hata laki 5 na unaweza ukafanya kitu kizuri, tuondoe huu ujinga wa director mkubwa na mdogo lets get creative watu waienjoy kazi. Congrats to Izzo and Nick hata kama video sijaona but I appreciate you efforts. Regards AJ”
Kumekuwepo na tabia iliyojengeka miongoni mwa baadhi ya wasanii, kutaja gharama kubwa zaidi ya ile halisi iliyotumika kuandaa video zao pindi wanapoulizwa gharama iliyotumika kukamilisha