Sep 24, 2014
Davido kushoot video mbili kwa mpigo wiki hii Marekani
Baada ya mastar wa Nigeria P-Square, Wizkid na Iyanya kuachia video zao mpya ambazo wote wameshoot Marekani hivi karibuni, hit maker wa ‘Aye’, Davido naye anatarajia kushoot video mbili kwa mpigo jijini New York, Marekani wiki hii.
Davido katumia facebook yake kuwatangazia dancers na warembo wa Marekani watakaopenda kushiriki kwenye video hiyo.
“Shooting 2 videos this week in NYC… Need amazing dancers,beautiful ladies for lead role & extras to come party with us… let’s ball and turn up for NEW YORK CITY one more time!…”
Mwanzoni mwa mwezi huu (September) Davido ambaye ameshinda tuzo nyingi mwaka huu ikiwemo BET, aliachia single mpya aliyomshirikisha Dj Arafat iitwayo ‘Naughty’.