Moja kati ya wasanii wakali wa Bongo Flava, Rich Mavoko amatease
video yake mpya anayotarajia kuiachia hivi karibuni ya wimbo wake
‘Pacha Wangu’. Mavoko aliyekuwa kimya kwa muda kidogo amesema mashabiki
wake na watu wengine wote wakae mkao wa kula kupokea kitu kipya na cha
utofauti kitakachoishangaza Afrika kiujumla kwakuwa safari hii amesema
anakuja kwa utofauti kidogo
.
“Wadau wakae mkao wa kula. Kuna video mpya itatoka wiki hii siku ya
Alhamisi. Ni video fulani ambayo sikupenda sana kuongea mambo mengi
kabla watu hawajaiona. Nataka watu waone kwanza halafu nitazungumza
mengi kuhusu nimefanya wapi na kwanini nimetoa wakati huu,” Mavoko
ameiambiawambura babu blog