Waandaaji wa Tamasha la Kiswahili Washington DC Ndugu Patrick Kajale na Dada Finiana wakijadili jambo na ndugu Safari ambaye ndiye Mtunzi wa kile kitabu Nambari moja Amazon cha Nyayo za Obama.
Patrick Kajale Mwandaaji wa Tamasha la Kiswahili
Afisa usalama wa ubalozi wa Tanzania Dr Mkama akiwa na baadhi ya maofisa wa ubalozi.
Maofisa wa ubalozi wakiendelea kula nyamachoma kutoka katika banda la Safari Restaurant DC
Nyama
Choma katika banda la Safari Restaurant Washington DC,Safari ni Mgahawa
wa Kitanzania uliopo katika jiji la Washington ambapo vyakula vingi
vya kinyumbani vinapatikana.
Mishikaki ikiendelea kuchomwa katika banda la Safari Restaurant kwenye Tamasha la Kiswahili
Watu wakiwa mstari kwenye banda la Safari wakijipatia nyama ya motomoto kutoka kwenye grill
Mabanda mbali mbali yakitangaza shughuli zao kwenye Tamasha la kiswahili
Warembo Wakareeeeezz kutoka washington DC na Texas pia walihudhuria Tamasha hili la Kiswahili
Ice Cream au lamba lamba kama zinavyojulikana kwa kiswahili pia zilikuwepo kwa ajili ya watoto na watu wazima
Miss Temeke- CEO wa Kwetu Fashion Design akiwa katika Meza yake baada ya kumaliza Maonyesho yake ya Mavazi ya Kitanzania.
Walimbwende hawa katika Mavazi ya Kwetu Fashion Design.
Nguo za kina Kaka kutoka kwetu fashion Design By Miss Temeke Patrick Kajale nae akipita katika Vazi la Kimasai
CEO Wa Kwetu Fashion Miss Temeke Akiwapungia Umati Baada yakumaliza Maonyesho yake ya Mavazi
Juu na chini ni watu mbali mbali wakiendelea kutazama mambo mbali mbali yaliyokuwa yakiendelea.
Kwa
Upande wa burudani walikuwepo pia Wasanii Mahiri wa kizazi Kipya
Wakitanzania na East Afrika kwa ujumla waishio Marekani kama AJ
Ubao,Prince Herry,Max na Jumbe Mr TZ Mwanadada "Senai" Mpiga Gitaa Maarufu kutoka Afrika Mashariki anayeishi Marekani
Mikono Juu..Prince Herry akiwarusha Watazamaji kwa Ufasaha na Style yake ya lay back.Prince Herry Akifokafoka kwa hisia kali katika kile kibao chake kinachoitwa "Au Sio"
Kijana Max Ambaye watu wengi wanamwita Silent Killer aliwarusha watazamaji vilivyoJumbe Mr Tanzania aliwarusha watazamaji kwa style yake yakipekee huku Mwanamuziki AJ Ubao akimsindikiza kwa nyuma
Je waukumbuka Mchezo gani huo?....Mwakani tutaweka pia Bao.
Kwa mara
ya Kwanza kabisa nchini marekani limefanyka tamasha la Kiswahili katika
jiji la Washington, likijumuisha nchi zote za Afrika Mashariki na kati
zinazozungumza lugha ya kiswahili.Tamasha hili liliandaliwa ili kuweza
kutangaza tamaduni za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Chakula,
Mavazi, Ngoma za Asili, Miziki ya Kizazi Kipya,na mambo mbali mbali ya
kiasilia.
Waandaaji
Wanatoa Shukrani Kwa watu wote waliojitokeza kwani hii ni mara ya
kwanza kabisa Tamasha kama hili kufanyika nchini Marekani hivyo
tutegemee Mambo mengi Makubwa Mwakani kwani Huu ni Mwanzo.