Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (kushoto) akizionesha kadi za Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) baada ya ukabidhiwa na Katibu wa Kata ya Lionja,
Wilayani Nachingwea, Hashimu Halifa (kulia). Waliorudisha kadi hizo na
kujiunga na CCM ni Lusia Mohammed, Abdu Ngawina na Mohammed Kindamba.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe akizungumza na Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za
CCM Kata ya Lionja, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee
katika Kata hiyo, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe
ambaye yupo katika ziara ya kikazi katika Jimbo lake la Nachingwea
aliwaomba wajumbe hao kuhakikisha chama kinaimarishwa zaidi na
kuwakaribisha wanachama wote wanaotoka vyama vingine ili wajiunge na
CCM.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (kulia) akizungumza na Mjumbe wa CCM Kata ya Lionja
ambaye ni mlemavu wa miguu, Hassan Chingwale baada ya kumaliza kikao
chake na Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa
Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo, Wilaya ya
Nachingwea mkoani Lindi.
(Picha na zote na Felix Mwagara).