MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Oct 9, 2014

Mkapa, Karume Wakacha Uzinduzi wa Katiba

Japokuwa jana niliangalia kwa muda mfupi Mchakato wa makabidhiano ya katiba ya CCM iliyooandaliwa na Sitta, Chenge,wabunge wengi wa CCM (ukiwaacha Lugola na Filikunjombe walioiasi) na mawakala wao, nilishtushwa kutowaona
Mabalozi wa nchi wafadhili wa serikali ya CCM, wajumbe wote wa Tume ya Katiba na Maraisi Wastaafu Mh Benjamin Mkapa na Aman Abeid Karume. Je, tatizo ni mimi sikuwaona au ni kweli hawakuwepo? Na kama ni kweli hawakuwepo;

Je, ndo tuamini kuwa watu wote hawa muhimu wamesusia katiba ya CCM?

Je, huu siyo uthibithisho wa taarifa kuwa mabalozi hawa walimwambia JK haiafiki katiba hiyo? 

Je, hii haimaanishi kuwa katiba ya fisadi Chenge na mbabaishaji Samwel Sitta inapingwa vikali hata ndani ya ccm yenyewe? 
Ninatafakari tu kwa sauti wala sina ugomvi na mtu ye yote. 

Nawasilisha, 
By Aweda 
CHANZO UDAKU SPECIAL.COM