MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Mar 13, 2015

Tanzania kuwa mwenyeji Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na wageni waliofika ofisini kwake kumjulisha kuhusu Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute litakalofanyika nchini Tanzania na kuhusisha nchi 18 tarehe 21 na 22 Machi mwaka huu. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, wakwanza kulia ni Bw. Ramadhani Madabida na anayefuata ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz.
Bw. Ramadhani Madabida (kulia) akifafanua jambo walipokutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara wakwanza kushoto kumpa taarifa ya Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni lililoandaliwa na Kilimanjaro Dialogue Institute litakalofanyika nchini Tanzania tarehe 21 na 22 Machi mwaka huu na kuhusisha nchi 18. katikati ni Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz.
Rais wa Kilimanjaro Dialogue Institute Bw. Ali Akkiz (wapili kulia) akielezea jinsi walivyojiandaa kufanikisha Tamasha la Kimataifa la Lugha na Utamaduni litakalohusisha nchi 18 walipokutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (wapili kushoto). Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, na kulia ni Bw. Ramadhani Madabida