Chiku Abwao akiwahutubia wananchi
CHAMA
cha ACT wazalendo kimezindua kampeni zake za ubunge katika jimbo
la Iringa huku mgombea wake ubunge katika jimbo hilo Bi Chiku
Abwao akivilalamikia baadhi ya vyombo vya habari nchini kwa kukalia
habari zake zinazohusiana na uchafu wa mgombea Urais wa chama
cha Demokrasia na maendeleo (chadema) anayewakilisha vyama vinavyounda
umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) Edward LOwassa kuwa hana sifa
ya kuwa Rais wa nchini hii.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kampeni zake juzi katika uwanja wa
Mwembetogwa mjini Iringa , Abwao alisema kuwa anasikitishwa na hatua
ya baadhi ya wanahabari na vyombo vya habari nchini kukalia pasipo
kuzitoa habari za kupinga hatua ya Chadema na ukawa kumsimamisha
Lowasa kuwa mgombea urais wakati wao kama wapinzani sera na
ajenda yao kubwa ilikuwa ni kupinga ufisadi na hata kumtaja
hadharani waziri mkuu huyo mstaafu kwenye orodha ya mafisadi .
"Kila
wakati nimekuwa nikikemea hatua ya Chadema na Ukawa kukumbatia
mafisadi wakubwa na hata kuwana nafasi za kuwania Urais ila leo
naomba kupeleka kilio changu kwa baadhi ya vyombo vya habari na
wanahabari hapa nchini ambao wamekuwa wakikalia habari zangu za
kupinga ufisadi na kutoafiki mgombea Urais wa UKAWA Bw
Lowassa......nikikemea sana masuala ya Lowassa kuhusishwa na ufisadi
papa na Chadema na leo kukaribishwa kugombea Urais wanahabari na
vyombo vya habari havitoi katika magazeti ninawasiwasi na wao
wanamshiko wa ufisadi nitasema ukweli kwa wale ambao wamemezwa na
ufisadi lakini si kwa wanahabari na vyombo vyote " alisema Chiku
Kuwa
baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii imekuwa ikitoa
habari zake pasipo kuficha ukweli ila wapo baadhi ambao wamekuwa
wakificha ukweli na yupo tayari kuendelea kupinga hatua ya UKAWA
kumsimamisha Lowassa kuwa mgombea huku akivitaka vyombo vya habari
kulisaidia Taifa kupata kiongozi bora na sio bora kiongozi.
"
Wapo baadhi ya waandishi wamekuwa wakiweka mambo wazi ila wapo
ambao wamemezwa na ufisadi ambao kazi yao ni kutetea ufisadi na kuwa
yupo tayari kusema kweli kwa faida ya watanzania "
Hata
hivyo alisema sababu ya yeye kuondoka ndani ya CHADEMA ni
kutokana na hatua ya chama hicho kumkaribisha waliyemuita fisadi
kuwa mgombea Urais na kuwaacha wanachama wenye sifa ya kuliongoza
Taifa .
Pasipo
kutaja majina ya wana chadema ambao walikuwa na sifa ya kuwania
nafasi ya Urais alisema kuwa kwa upande wake alikuwa ni mbunge wa
viti maalum na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema ila kutokana na
kukaribisha watu wachafu kugombea nafasi hiyo ya Urais hakupenda
kubaki ndani ya chama hicho na hivyo kulazimika kujiunga na ACT
wazalendo chama chenye misingi bora ya uongozi.
Bi
Abwao alisema kuwa kuna haja ya wananchi kutomchagua Lowasa na pia
kwa wana Iringa mjini kutoendelea kuburuzwa na aliyekuwa mbunge wa
jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa ambae aliusadikisha umma
kuwa Lowassa ni fisadi na kuwa angewashangaa watanzania ambao
watasimama kumshangilia Lowassa na hata kudai kuwa watu hao
wangepaswa kupimwa akili ila leo yeye na viongozi wenzake wa UKAWA
wamekuwa wa kwanza kumpigia kampeni na kunadiwa na huyo waliyemuita
ni fisadi hata bila ya kwenda kupima akili zao.
Alisema
kuwa lazima wananchi kukwepa kuwachagua viongozi wanaotafuta
ungozi kwa pesa na badala yake kuchagua viongozi makini kutoka
chama chake cha ACT Wazalendo ambacho hakina ubia na mafisadi .
Kuhusiana
na nini chama chake kitafanya iwapo wananchi wa jimbo la Iringa
mjini watamchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo alisema ni pamoja na
kuweka mfumo mzuri wa kuwasaidia wazee kwa kuwakatia bima za afya ,
kuanzisha miradi ya vijana na kusaidia yatima na walemavu
kiuchumi.
Kwani
alisema mbunge aliyekuwepo jimbo hilo Mchungaji Msigwa amechangia
kuua nguvu ya upinzani katika jimbo hilo kutokana na kushindwa
kutimiza ahadi ambazo alipata kutoa kwa wananchi mwaka 2010 japo
ameomba wananchi kumwamini yeye kwa kumchagua kuwa mbunge wa
jimbo hilo japo kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na iwapo
atashindwa kutimiza ahadi zake kama alivyofanya mchungaji Msigwa basi
wasimchague tena mwaka 2020.
Na MatukiodaimaBLog