Mke
wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi
wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua mumewe Dkt John Pombe Magufuli
kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya
tano,kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa wa Oktoba 25 mwaka huu.
Mara
bada ya kuhutubia chumba chetu cha habari kilihemewa na simu za wadau
mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kuelezea furaha yao sio tu kwa
kumuona jukwaani bali pia kwa kuongea kwa kujiamini. Mama Magufuli
amekuwa haonekani sana kwa sababu ya kuuguza mgonjwa nyumbani kwao
Chato. Wamesema wametiwa moyo sana na haiba ya Mama Magufuli na
wameshangazwa kwa uwezo wake mkubwa wa kuongea mbele za watu bila woga
na bila kumung'unya maneno.
Mke
wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi
wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu.
|
Mke
wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akipeana mkono na
Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mara baada ya
kuwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt
Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano
|
Wananchi
wa Chato wakimshangilia Mama Magufuli kwa shangwe kwenye mkutano wa
hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato
mkoani Geita.