Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa Maadhimisho ya Siku
ya Bahari Duniani, uliofanyika Kitaifa mkoani Mtwara,leo mchana, wakisikiliza
mada mbalimbali zinazohusu changamoto na mikakati ya kuboresha mazingira ya
Usafiri wa Majini.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, akitoa shukrani zake kwa Ushirikiano
unaoonyeshwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar katika sekta ya Uchukuzi kabla hajamkaribisha
Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano kufungua rasmi Mkutano wa
Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika mkoani Mtwara,leo
mchana.
Mkurugenzi
wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande,
akifafanua jambo katika Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani,
uliofanyika mkoani Mtwara, leo mchana.
Mkuu wa Kikosi cha Meli Vita (701 KJ),
TPDF-NAVY, Brigedia Generali, Richard Makanzo, akifafanua jambo, leo mchana
katika Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika Kitaifa
mkoani Mtwara, leo mchana
Naibu Waziri wa Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Zanzibar, Issa Usi Gavu, akifungua
rasmi Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani, uliofanyika mkoani
Mtwara,leo mchana.Maadhimisho ya Siku ya Bahari yanafanyika Kitaifa Mkoani
Mtwara kwa siku tatu.
(Habari
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)