Wanunuzi wa madini wakikagua madini ya vito kutoka kwa
mfanyabiashara wa madini wa Tanzania katika banda la Tanzania kwenye maonesho
kimataifa ya 56 ya Madini ya vito na usonara yanayofanyika mjini Bankok,
Thailand.
Ofisa kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), Bi.
Stella akimpatia maelezo mmoja kati ya wanunuzi wa madini ya vito waliofika
katika banda la Tanzania kutaka maelezo ya jinsi ya kuweza kununua madini hayo
ya vito yanayopatikana Tanzania.
Picha ya pamoja kati ya ujumbe kutoka Wizara ya Nishati na
Madini ya Tanzania na maofisa waandamizi wanaosimamia maonesho ya kimataifa ya
Madini ya vito mara baada ya ufunguzi rasmi kufanyika jijini Bangkok, Thailand.
Wanunuzi wa Madini ya vito waliofika katika banda la Tanzania
wakipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini waliopo
kwenye banda la Tanzania.
chanzo: JIACHIE