Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Africommerce International Limited,
Elisante Muro wakati wa kikao cha kujadili fursa za uwekezaji.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)
akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Africommerce International Limited, Elisante Muro (hayupo
pichani) ambaye alimtembelea Waziri huyo kuzungumzia fursa za uwekezaji
kwenye sekta ya nishati nchini. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu-
Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo akifuatiwa na Naibu Katibu
Mkuu- Madini, Profesa James Mdoe.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)
akizungumza jambo wakati wa kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Africommerce International Limited, Elisante Muro (hayupo pichani)
wakati wa kikao cha kujadili fursa za uwekezaji. Katikati ni Naibu
Katibu Mkuu- Madini, Profesa James Mdoe na wa kwanza kulia ni Naibu
Katibu Mkuu- Nishati, Dkt. Mhandisi, Juliana Pallangyo.
WAZIRI wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Africommerce International Limited, Elisante Muro
na kuzungumzia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini hususan katika
sekta ya Nishati.
Muro alimtembelea Waziri Muhongo na kueleza nia ya Kampuni yake
kuwekeza kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta kutoka
Dar es Salaam hadi Mwanza na vilevile uwekezaji kwenye mradi wa ujenzi
wa nguzo za umeme za zege.