Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Johannes
Msumule akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni alizungumzia
hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi na kufanya
kazi nchini kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni, wakati wa mkutano wa
kuzungumzia hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi
nchini na kufanya kazi kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao
Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).