Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) imesema itaendelea kupambana
na wale wote watakaogundulika kwa wizi wa kazi za sanaa.
Agizo hilo limetolewa na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo
Alphayo Kidata alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari na kueleza kuwa
wapo katika operesheni ya kukamata wezi wa kazi za sanaa .
"Ipo kamati ambayo inajumuisha
wadau kama Bodi ya Filamu, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na COSOTA ikishirikiana
na Jeshi la Polisi katika kupambana na
wizi wa kazi za wasanii unaokidhiri siku hadi siku' `Alisema Kaimu Kamishna Kidata.
Serikali ipo makini kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania
katika kukusanya mapato hasa kuongeza maeneo ya kukusanya mapato ikiwemo eneo
la kazi za sanaa hivyo Serikali haitakubali kuona inakosa mapato hayo na
yoyote anayejua mtu au kikundi cha watu kinachofanya wizi wa kazi za sanaa
atoe taarifa ofisi za TRA.