Spika
Rebecca Kadaga (Mb) wa Uganda afunga Warsha ya siku mbili ya
Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika
Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola
Kanda ya Afrika kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakichangia mada katika
Warsha kuhusu ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi za maamuzi wakati
wa siku ya ufungaji warsha hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam 21-23
Januari, 2016.(Picha zote na Benedict Liwenga)
Na Benedict Liwenga.
SPIKA
wa Bunge la Uganda, Mhe. Rebecca Kadaga (Mb), ambae pia ni Mwenyekiti wa
CWP Kimataifa amezihasa nchi Wanachama wa Sekretarieti ya Chama cha
Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuendelea kuwathamini
wanawake kwa kuwapa vipaumbele vya ushiriki katika ngazi za maamuzi
pamoja na kuwaenzi wanawake waliotoa mchango wa maendeleo ya nchi zao.
Spika
Kadaga ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akifunga rasmi
Warsha ya siku mbili iliyohusu kujadili ushiriki wa wanawake katika
ngazi za maamuzi ili kubuni mbinu na mikakati ya kuongeza idadi ya
Wanawake katika ngazi za siasa na kijamii.
Mhe.
Kadaga ameeleza kuwa, nchi Wanachama hazinabudi kuthamini mchango mkubwa
wa wanawake katika masuala ya kijamii pamoja na kisiasa, hivyo kuna
haja ya kuwaenzi kwa kutunza nyaraka zao muhimu ikiwemo kuwaendeleza
wanawake kielimu ili kuweza kuleta maendeleo katika nchi husika.
“Ni
vema tukaaangalia mchango mkubwa unaotolewa na Wanawake katika nchi zetu
hususani katika masuala ya kijamii pamoja na kisiasa, basi nchi zetu
hazinabudi kuwajali kwa kuwashirikisha katika ngazi zote muhimu ili kuwe
na usawa kati ya wanawake na wanaume, lakini pia kuna haja ya jamii
husika kuwaelimisha wanawake hawa ili waweze kuleta mchango mkubwa
katika jamii zetu”, alisema Spika Kadaga.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika,
Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) kutoka Afrika Kusini, amezidi kuipongeza
Tanzania katika hatua nyingine kwa kujali haki na usawa katika masuala
ya kisiasa ambapo pia ameimwagia sifa kwa uchaguzi uliopita wa mwaka
2015 kuwa wa huru na haki na kuzitaka nchi nyingine za Afrika kufanya
chaguzi zake kuiga mfano huo.
Kwa
upande wao Wajumbe wa Warsha hiyo wameendelea kujadili masuala
mbalimbali ambayo yanaweza kuleta mabadiliko katika jamii kwa
kuhakikisha kuwa wanawake wanapewa fursa sawa na wanaume katika masuala
ya kisiasa na kijamii ambapo msisitizo mkubwa unaotolewa katika warsha
hiyo ni ‘ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi’.
Sambasamba
na hilo, suala la kuwashirikisha wanawake kwa njia ya Vyombo vya habari
na mitandao ya kijamii limezungumziwa katika warsha hiyo ambapo
msisitizo umetolewa wa kutumia mitandao hiyo kwa njia ya kuelimisha umma
juu ya nafasi ya mwanamke katika ngazi za maamuzi ambapo endapo
ikitumiwa vema inaweza kuleta usawa katika jamii.
Nchi zilizoweza kushiriki katika Warsha hiyo ni Tanzania, Uganda, Kenya, Ghana, Nigeria, Zambia, Mauritus pamoja na Afrika Kusini.
Nchi zilizoweza kushiriki katika Warsha hiyo ni Tanzania, Uganda, Kenya, Ghana, Nigeria, Zambia, Mauritus pamoja na Afrika Kusini.