Meneja wa wasanii wa bongo
fleva maarufu kwa jina la Meneja Maneno, amefunguka na kusema wapo
wasanii wengi Bongo wanaamini ushirikina na kukiri kuwa wapo wasanii
wengine ambao yeye mwenyewe aliwapeleka kwa waganga wa kienyeji kwa
ajili ya kuroga. Meneja Maneno aliyewahi kuwa meneja wa
Diamond Platnumz, Rich Mavoko, Sam wa Ukweli na Nay wa
Mitego, amefunguka hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa
Radio na kuwataja wasanii ambao aliwahi kuwapeleka kwa waganga na ambao
wanaamini sana ushirikina kuwa ni pamja na Rich Mavoko, Sam wa Ukweli huku akisema katika wote Diamond Platnumz ndiyo zaidi yao.
"Ndele ni sehemu ambayo
baadhi ya wasanii waliiamini sana lakini Mungu akisema 'Yes' ni 'Yes' tu
kwa hiyo nakumbuka wasanii ambao nilikwenda nao kwa waganga kuroga ni
pamoja na Rich Mavoko tena tulienda mbali kabisa huko Kigamboni ndani
ndani huko tumeenda ndugu yangu, nilisharusha nazi katikati yaani usiku
ule unajifanya chizi kama umevurugwa" alisema Meneja Maneno
Meneja Maneno
Meneja Maneno aliendelea kutoa orodha ya
wasanii hao ambao kwao shiriki ni kitu ambacho wanakiamini na kukiri
kwenda nao huko na kufanya mambo hayo
"Hata Sam wa Ukweli siwezi
kukataa, ni watu ambao imani yao iliwapeleka huko lakini mimi nakumbuka
kazi yangu niliyokuwa nafanya sikutaka kwenda kwa waganga.... ila sasa
huyu Mondi sasa nimepata taabu naye, mara leo twende kwa mjomba,
tunapeleka unga, leo tunapeleka mchele na mganga alivyo mshenzi hajawahi
kuagiza samaki, yeye ni jogoo, mbuzi" alisisitiza Meneja Maneno