MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

May 27, 2017

Waislamu watakiwa kudumisha amani


Muft wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubery
 Waumini wa dini ya kiislamu nchini wametakiwa kuutumia vizuri mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kufanya matendo mema pamoja na kudumisha amani ndani ya taifa la Tanzania
Wito huo umetolewa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry Ally wakati akizungumza na Hotmix ya EATV kuhusu kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na kusema kuwa katika kipindi hiki waislamu wanapaswa kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo wakiwemo, yatima na watu wengine.
“Nchi ikikosa amani hata shughuli nyingine za maendeleo na ibada haziwezi kufanyika kama inavyopaswa, hivyo basi ni muhimu kwa waislamu nchini kuwa mfano wa kudumisha amani na upendo”. Alisema Mufti
Sheikh Zubery, ameongeza kuwa katika mwezi huo Mtukufu wa Ramadhan Waislamu wanatakiwa kuishi kwa mapenzi na upendo, ikiwa ni pamoja kuwangalia na kuwasaidia wale wasiokuwa na uwezo wakiwemo, mayatima na watu wengine wasiojiweza.
Katika hatua nyingine naye, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum amewasihi waislamu kiujumla kuutumia mwezi mtukufu wa Ramadhan katika kuiombea nchi pamoja na kusameheana kwa waliokoseana bila ya kusahau kutoa misaada kwa watu wasiojiweza.

Ni fainali ya kihistoria Kombe la Shirikisho

Simba SC ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza leo zinakutana Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye fainali za kuwania Kombe la Shirikisho l katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni. Tayari timu zote ziko mjini Dodoma na zimekuwa zikirushiana tambo za hapa na pale, wakati Simba wakiwa wamekamia kutwaa kombe hilo ili kujihakikishia ushiriki katika miachuano ya Kimataifa ambayo imeikosa kwa miaka takriban mitano.
Kwa upande wa Mbao, wao wanataka kuweka historia mpya katika soka la Tanzania kuwa timu ya kwanza kupanda daraja kwa 'Mlango wa Nyuma' na kisha kufuzu michuano ya Kimataifa.
Mshindi wa mchezo wa fainali (Kwa msimu huu kati ya Simba na Mbao), ndiye akayekuwa Bingwa wa Kombe la ASFC - HD, atapewa Kombe la Ubingwa na zawadi ya fedha kiasi cha shilingi milioni hamisini (50,000,000/-) kama zilivyoainishwa kwenye waraka wa zawadi wa michuano.

Wasanii vinara kwa ushirikina watajwa

Meneja wa wasanii wa bongo fleva maarufu kwa jina la Meneja Maneno, amefunguka na kusema wapo wasanii wengi Bongo wanaamini ushirikina na kukiri kuwa wapo wasanii wengine ambao yeye mwenyewe aliwapeleka kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kuroga. Meneja Maneno aliyewahi kuwa meneja wa Diamond Platnumz, Rich Mavoko, Sam wa Ukweli na Nay wa Mitego, amefunguka hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kuwataja wasanii ambao aliwahi kuwapeleka kwa waganga na ambao wanaamini sana ushirikina kuwa ni pamja na Rich Mavoko, Sam wa Ukweli huku akisema katika wote Diamond Platnumz ndiyo zaidi yao. 
"Ndele ni sehemu ambayo baadhi ya wasanii waliiamini sana lakini Mungu akisema 'Yes' ni 'Yes' tu kwa hiyo nakumbuka wasanii ambao nilikwenda nao kwa waganga kuroga ni pamoja na Rich Mavoko tena tulienda mbali kabisa huko Kigamboni ndani ndani huko tumeenda ndugu yangu, nilisharusha nazi katikati yaani usiku ule unajifanya chizi kama umevurugwa" alisema Meneja Maneno
Meneja Maneno
Meneja Maneno aliendelea kutoa orodha ya wasanii hao ambao kwao shiriki ni kitu ambacho wanakiamini na kukiri kwenda nao huko na kufanya mambo hayo 
"Hata Sam wa Ukweli siwezi kukataa, ni watu ambao imani yao iliwapeleka huko lakini mimi nakumbuka kazi yangu niliyokuwa nafanya sikutaka kwenda kwa waganga.... ila sasa huyu Mondi sasa nimepata taabu naye, mara leo twende kwa mjomba, tunapeleka unga, leo tunapeleka mchele na mganga alivyo mshenzi hajawahi kuagiza samaki, yeye ni jogoo, mbuzi" alisisitiza Meneja Maneno 

May 26, 2017

HII NDIO SABABU MUNGU BADO ANALIPENDA TAIFA LA TANZANIA.

Tanzania ni nchi pekee zaidi duniani inayotajwa kwa mambo mengi mazuri na yenye kutia moyo. mataifa mengi duniani yamekuwa yakiwa katika migogoro mingi tabu nyingi sana hivyo Tanzania imekuwa kama nchi moja wapo duniani zilizopewa kipaumbele na Mwenyezi Mungu kwa mali nyingi yaani utajiri wa Madini, gasi na maziwa na bahari na hifadhi au mbuga za wanyama hivyo ni jambo pekee la kujivunia kama watanzania  na tunapaswa kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kila namna anayozidi kutuwezesha na kuzidi kutupatia maalifa zaidi.

Mabali na hapo Tanzania imekuwa na viongozi makini wasiopenda mabaya viongozi wanaolipenda Taifa lao kama wazalendo wakiwemo waasisi wa Taifa hili Hayati baba wa Taifa mwalimu julius kambarage nyerere na viongozi wengine na watawala kwenye kila kona ya nchi hii ya tanzania. kuna mambo mengi sana bado yamefichika ndani ya nchi hii lakini kwa uweza wa Mungu wetu mambo haya sas yanaanza kuonekana na matunda yake tunayaona na tunaanza kuyafurahia.  tukikumbuka vizuri Taifa hili limeshawahi kuwa n wasisi mbalimbali katika vitengo tofauti na kulifanya taifa hili kuwa na msimamo thabiti mpaka hapa tulipofikia. moja ya mambo haya ni NEMBO YA TAIFA la Tanzania ni nembo pekee duniani yenye picha ya binadamu wa KWANZA ambao ni Adamu Na Eva ikiwa kama ni ishara ya kumpa Mungu Toleo kwa watu wake wa kwanza hivyo ni jambo jema zaidi tunalipoaswa kulishukuru kila siku tunapoamka na hii ndio sababu kubwa ya Taifa hili kushikiliwa n Mungu na kutuepusha na mambo mabaya zaidi maana hata nembo yetu tu inaonesha kila kitu ambacho mMwenyezi Mungu alikiweka duniani na sisi tukakiweka kama alama ya ukumbusho kwake pasipokujua kama tunafanya hivyo na ndiomaana mpaka sasa Hata mvumbuzi wa nembo hii ya Taifa bado Yu Hai ni kwasababu ya mapendo ya Mungu wetu Mkuu.

Kuna Mambo kadha wa kadha ambayo TaifA la Tanzania linapaswa kujivunia ikiwa ni pamoja na sifa ya kudumisha Amani na upendo, kuwapokea wageni na kuwapa hifadhi pindi wanapopata matatizo katika nchi zao kutokana na migogoro ya kisiasa na uchu wa madaraka pia Tanzania imekuwa mstari wa mbele kusaidia kusruhisha migogoro hiyo ya mataifa mengine Africa na Duniani kwani ndio Nguzo pekee tuliyopewa na Mwenyezi Mungu. Viongozi wetu makini wapo kwaajili ya kufanya Taaifa hili liendelee zaidi kwani moja ya misimamo iliyowekwa na waasisi wetu hapoa awali ilikuwa ni kuwaweka watanzania wote karibu na waongee lugha moja na sio kubaguana kwa dini au kwa makabila ni jambo baya sana kwa Taifa lolote linapoanza kubaguana katika misingi ya kidini au kikabila huleta migongano mwisho wake huwa ni vita na tabu nyingi maana kunakuwa hakuna wa kumsaidia mwenzake wala hakuna masikilizano hivyo jambo ku8bwa ni kuzidi kuliombea Taifa letu la Tanzania na Mungu atazidi kutubariki na tuwaombee viongozi wetu wote wazidi kutuongoza vizuri na kufikia hatua ambayo kila mmoja wetu anapswa kuifikia.

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Watu 4 wafariki kwa kufukiwa na kifusi Geita

Moja kati ya machimbo ya dhahabu mkoni Geita
Watu wanne wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kufukiwa na kifusi katika machbo ya Nyamalinde kijiji cha Sobola nje kidogo ya wilaya ya Geita, mkoani Geita. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo limetokea leo majira ya saa mbili asubuhi katika machimbo hayo yanayomilikiwa na wananchi licha ya kuwa tayari yalishapigwa marufuku kuendelea kwa kazi hiyo.
Mponjoli amesema tukio hilo limetokea baada ya watu 7 kuingia ndani ya mgodi huo, lakini muda mfupi baadaye kifusi kikawaangukia na kusababisha vifo vya watu wanne kati yao huku watatu wakitoka salama licha ya kuwa na majeraha.
Amewataja watu waliopoteza maisha kuwa ni pamoja na Robert Kazegemwa, Jeremia Emmanuel, Makenya Mwita na Julius Timotheo.
Waliojeruhiwa ni pamoja na Mashaka Samuel, Justine Safari na Maneno Lusika ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Katoro.
Katika tukio lingine, leo majira ya saa 7 mchana tetemeko dogo la ardhi limetikisa katika mkoa wa Geita ambapo licha ya kutokuwa na madhara yoyote, limezua taharuki katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika shule ya sekondari Nyang'wale.
Kamanda Mponjoli amesema katika shule hiyo, wanafunzi walikuwa katika mitihani na ndipo walipokimbia kutoka darasani ili kujiokoa ambapo kutokana na msukumano, mwanafunzi mmoja alijeruhiwa lakini tayari amekwishapatiwa matibabu na yuko salama

Kila Mtanzania amshukuru Magufuli - Mabula

Stanslaus Mabula (Kulia), Rais Magufuli (kushoto)
Mbunge wa jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula amefunguka na kuwataka Watanzania kumshukuru sana Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na maamuzi yake aliyofanya jana kuhusiana na sakata la usafirishaji wa mchanga na madini. 
Mabula amesema Rais Magufuli anastahili kupongezwa na kila Mtanzania kwa jambo hilo kwani miaka mingi serikali imekuwa ikipoteza mapato na kupata hasara kutokana na mambo haya.
"Makontena haya zaidi ya miambili mpaka miatatu kusafirishwa nje yaani hapo serikali imepata hasara kubwa sana, unajua mimi ni Mjumbe wa Kamati ya PAC na mara kadhaa wamekuwa wakiomba mikataba ya madini ikaguliwe sasa haya ndiyo matokeo Mh. Rais alitambua na alizungumza sana kwenye kampeni yake kabla hajafika kwenye masuala ya kuangalia mikataba uchunguzi unajibiwa kwa uchunguzi. Kwa hiyo uchnguzi huu ni sahihi kwenda kufumua mikataba na kuona wapi tulipoanguka na wapi tunataka kwenda kwa ajili ya maisha ya Watanzania" alisistiza Mabula 
Mabula aliendelea kufafanua kuwa 
"Ukifanya mahesabu ya haraka haraka ambazo wataalamu wa hesabu wamekuwa wakizungumza baada ya Rais Magufuli kufanya maamuzi jana inaonekana karibia nusu ya bajeti ya serikali kwa mwaka mzima inapotea, sasa unaweza kuona kiasi gani cha fedha hizi zimekuwa zikipotea na sasa hivi tunafikiria kutumia tilioni 31 lakini karibia tilioni tisa tunataka kuzipata kutoka kwa wahisani kumbe tilioni tisa zinapotea kwenye mikono yetu, kwa hiyo yote haya inaonyesha jinsi gani Rais wetu anataka kutupeleka sehemu nzuri" alisisitiza Mabula 

Serikali kusimamia matibabu ya mzee Ngosha

Dkt. Hamis Kigwangalla na Francis Maige Ngosha ambaye ni mmoja wa wachora nembo ya taifa, alipomtembelea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Serikali ya imelazimika kumuhamishia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mzee Francis Maige Ngosha aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Amana kwa kipindi cha siku moja kwaajili yakupatiwa matibabu zaidi. Akitoa tamko la serikali Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Khamisi Kigwangalla amesema mzee huyo ambaye ni mmoja wa wachora Nembo ya Taifa amesema wameamua kumuhamishia katika hospital hiyo ya Taifa Muhimbili ili kufanyiwa uchunguzi wa kina na wataalamu wa magonjwa mbalimbali ili kubaini na kutibiwa.
Dkt. Kigwangalla amesema serikali itahakikisha inampa tiba kamili na malezi kwa kuzingatia haki ya kuishi ya binadamu na kuthamini mchango wa wazee na waasisi wa taifa.
Kwa upande wake daktari bingwa wa magonjwa ya dharura kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga amesema wanasubiri majibu ya vipimo wanavyomchunguza na pindi watakapobaini tatizo atapatiwa matibabu yake.
Kwa upande wake Francis Maige Ngosha ambaye ni mmoja wa wachora Nembo ya Taifa ameishukuru serikali na jami iliyokuwa ikimlea kwa miaka yote bila malipo.
Nembo ya Taifa

Rungu la Bodi ya Mikopo latua Dawasco


Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB) imetangaza azma ya kuifikisha mahakamani Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco) kama isipolipa deni lake la shilingi milioni 124 ndani ya siku 7
Hiyo ni fedha ambayo Dawasco wanadaiwa na bodi hiyo ikiwa ni malimbikizo ya makato ya wadaiwa ambao Dawasco imewakata lakini imeshindwa kuyawasilisha katika bodi hiyo
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Madeni kutoka Bodi ya Mikopo amesema Dawasco wametenda kosa kisheria kushindwa kuwasilisha fedha hizo licha ya kuwa wamekwishawakata waajiriwa wanaodaiwa na bodi hiyo.
Pia ametoa onyo kwa waajiriwa wa mashirika, taasisi, na makampuni mbalimbali kuhakikisha kuwa wanawasilisha fedha hizo kwa wakati bila kufuatiliwa na bodi.
Tangu kufanyika kwa mabadiliko ya kisheria ya kiwango cha makato kutoka asilimia 8 hadi asilimia 15, bodi ya mikopo imeweza kukusanya shilingi bilioni 12 kwa mwezi mmoja pekee kutoka kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa mwezi kabla ya kubadilika kwa kiwango hicho cha makato.

RC Shinyanga azuiwa kuingia mgodini

Zainab Tellack, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack, umezuiwa kuingia katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu alikokwenda kukagua iwapo uzalishaji unaendelea bila kuwepo kwa Maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini, TMAA.
Maofisa wa TMAA waliondoka mara baada ya ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu kukabidhiwa kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli hapo jana ikulu jijini Dar es sallaam.
Bi. Zainabu amesema ameagiza Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi huo kuhakikisha hakuna mtu anayetoka wala kuingia
Mapema leo Mkuu huyo wa Mkoa alitembelea mgodi mwingine wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia kama ulivyo ule wa Bulyanhulu.
Katika mgodi wa Buzwagi, Bi. Zainab na msafara wake waliruhusiwa kuingia na kushuhudia shughuli za uchimbaji zikiwa zimesitishwa kwa kukosekana maofisa wa TMAA walioondoka mara baada ya Rais Magufuli kutangaza kuvunja bodi na kutengua uteuzi wa watendaji wakuu wa wakala hiyo.

May 25, 2017

Yanga yatoa neno tuzo ya Msuva na Niyonzima

 Klabu ya Yanga SC imewapongeza wachezaji wake Saimoni Msuva na Haruna Niyonzima kwa kuondoka na tuzo katika hafla ya ugawaji tuzo za Ligi kuu Tanzania Bara katika msimu uliomalizika wa 2016/17.
Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Idara ya habari na mawasiliano ya klabu hiyo kwa kusema wanajivunia wachezaji hao kupata tuzo hizo kwani mafanikio ni chachu katika kuendelea kufanya vizuri katika mashindano yao kiujumla.
"Uongozi wa klabu ya Yanga SC pamoja na benchi la ufundi unatoa pongezi za dhati kwa wachezaji wetu Saimoni Msuva aliyeibuka mfungaji bora wa ligi kuu pamoja na Haruna Niyonzima aliyenyakua tuzo ya mchezaji bora wa kigeni ....Mafanikio yenu ndio chachu ya mafanikio ya klabu yetu....Tunajivunia hilo sambamba na wenzenu wote kwenye kikosi kwa kujituma kwa moyo wote kuhakikisha timu yenu inakuwa mabingwa wa ligi kuu mara tatu mfululizo". Ilisema taarifa hiyo
Niyonzima ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda Method Mwanjale kutoka Simba na Yusuph Ndikumana wa Mbao FC huku Saimon Msuva akiwa sawa na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting baada ya kuwa na idadi sawa ya magoli msimu huo.

Tutanyolewa bila maji - Tundu Lissu

Tundu Lissu
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu ameibuka na kuishauri serikali jambo la kufanya kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliofanywa na kamati ilyoundwa na Rais John Magufuli.

Tundu Lissu anasema Tanzania ni mwanachama wa 'The MIGA Convention' hivyo ukiwa mwanachama ukachukua mali za wawekezaji wao utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa na kwenda kushughulikiwa huko, hivyo Tundu Lissu ametoa ushauri wa namna nzuri ya kushughulika na watu 
"Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa 'The MIGA Convention' Multilateral Investment Guarantee Agency ya benki ya dunia, ukiwa mwanachama wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukichukua mali zao kama walivyochukuliwa mali zao namna hii utapelekwa kwenye mahakama zao za kimataifa unaenda kushughulikiwa huko, tumesaini mkataba wa ulinzi wa wawekezaji na mataifa wanayotoka wawekezaji hao Marekani, Canada, Uingereza wote ni mabosi wakubwa makampuni ambayo Rais ameyakamatia mali zao yanatoka kwenye hizi nchi tuna 'bilateral investment treaties ambazo zinalinda mikataba hii" alisema Tundu Lissu 
Makontena ya mchanga wenye madini yaliyozuiliwa bandarini
Tundu Lissu anasema hili suala tusipokuwa makini nalo linaweza kuleta matatizo makubwa huku akimtaja muhusika wa mikataba iliyolifikisha taifa katika hasara iliyobainika katika uchunguzi huo.
"Rais anajiingiza kwenye mgogoro mkubwa, akimkamata Dalali Kafumu peke yake, tutamwambia kwanini siyo Gray Mwakalukwa mikataba yote hii imeingia wakati wa Mr. Gray Mwakalukwa, kwanini siyo Daniel Yona, kwanini siyo Jakaya Kikwete sababu alikuwa Waziri na mimi nina mkataba wa Bulyankulu na kwanini siyo mawaziri wote, kwa sababu mikataba iliingiwa wakiwa mawaziri" alisema Tundu Lissu 
Rais Magufuli akipokea ripoti ya kamati 
Lakini mbali na kusema yote hayo Tundu Lissu alitoa ushauri wake katika suala hilo...
"Kama unataka kufanya haya unayoyafanya elewa hali halisi ilivyo, tatizo liko wapi kama tatizo ni kwamba tunapata mapato kidogo na kweli wanatupiga kweli kweli ila kama utaka kufanya mambo kweli kweli kajiondoe kwanza MIGA ili hao wawekezaji wasikushtaki kwenye hizo mahakama za huko, maana wakikushtaki kule unanyolewa bila maji, hakuna ndege ya Tanzania itakanyaga hizo nchi wataikamata, hakuna hela tutaweka kwenye nanii za kimataifa watazikamata, kwa sababu tunavunja mikataba ya kimataifa inayolindwa na sheria za kiwekezaji za kimataifa, kwa hiyo anzia huko juu ukimaliza mikataba ya kimataifa, njoo kwenye mikataba kati ya nchi na nchi ondoa hiyo mikataba ukishaondoa hiyo hushtakiki nje, baada ya hapo njoo ndani sababu bado unaweza kushtakiwa ndani" alisisitiza Tundu Lissu

VIDEO: Chadema hawana Shukrani - Wolper


 Wolper na baadhi ya Wasanii wakati wa kampeni za Uchaguzi mkuu 2015.
Malkia wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amefunguka sababu za kuacha kuendelea kuisapoti CHADEMA ni viongozi wa chama hicho kushindwa kuutambua mchango wake alioutoa wakati wa uchaguzi mkuu hali iliyomfanya ajihihisi mpweke na kama ametelekezwa
Ikiwa ni mara ya kwanza Wolper kufunguka ishu hiyo katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kwenye ukurasa wa facebook EATV, amesema hajawai kuwa msaliti kwani hakuwa mwanachama wa chama hicho lakini alisikitishwa na uongozi wa chama kushindwa hata kumshukuru kwa kazi aliyoifanya wakati wa uchaguzi mkuu kwa kujitoa pasipo kulipwa hata shilingi elfu 10 za kitanzania.
Pamoja na kuwa alifanya kampeni za kumsapoti Mgombea uraisi kupitia mwamvuli wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa, Wolper amedai kuwa hakuwa anasapoti chama kizima bali mgombea kwa kuwa yeye ni shabiki wa kiongozi huyo na familia yake kwa ujumla ndiyo maana hakukubali kulipwa katika kampeni hizo.
Wolper akiwa Kikaangoni
 "Mimi nilifanya siasa kwa sababu namkubali Lowassa, na mimi ni shabiki wake na familia yake kwa ujumla. Nilianza kumsapoti Lowassa tangu yupo CCM. Mimi ni mfanyabiashara na muigizaji, sijawahi kuwa mwanasiasa ndio maana nilikuwa namsapoti mtu mmoja mmoja na siyo chama. Hata hivyo mimi siyo Yuda kwa CHADEMA kwa sababu sijawahi kuwa mwanachama wao na sina chama  chochote lakini wao baada ya uchaguzi walinitelekeza kiasi cha kunifanya nijisikie mpweke. Hata kama hawakushinda uchaguzi walipaswa hata viongozi wawili wanishukuru tu kwa maneno ili na mimi nipate faraja lakini hawakuweza kufanya hivyo.
Hata hivyo Wolper amekiri wazi hata tatizo na Mhe Lowassa na hawezi kuml;aumu kwa yaliyotokea bali atakuwa naye bega kqwa bega tena kumsapoti endapo atapata tena nafasi ya kugombea urais 2020.
Mtazame hapa chini Wolper akifunguka kwa undani zaidi.

Mtavimba matumbo Dar es Salaam - Musukuma


Joseph Kasheku, Mbunge wa Geita
Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Musukuma amesema hawezi kumsifia hata kidogo Prof. Jumanne Maghembe, Waziri wa Maliasili na Utalii kwani yeye na watu wake wa Wizara wanafanya mambo ya ajabu hasa kwa watu wa Kanda ya Ziwa.

Musukuma anasema watu wa Wizara ya Maliasili wamekuwa wakiuza ng'ombe za watu jamii ya wasukuma na kuzipiga mnada kwa dili kwa lengo la kujinufaisha wenyewe, hivyo mbunge huyo amesema wasukuma wameamua kuwa wataziroga ng'ombe zote ili wanaokula ngo'mbe hizo Dar es Salaam wavimbe matumbo. 
"Napata shida sana kujiuliza labda sisi watu wa kanda ya ziwa labda tulikuja kwa bahati mbaya Tanzania hii, mbona yanayofanyika Kanda ya Ziwa hayafanyiki Kanda ya Kaskazini wakati nao wana mapori, Waziri ametoa siku tatu tukamatiwe ng'ombe kwa kisingizio kwamba ni ng'ombe za Wanyarwanda wakati huo huo watumishi wake wanaowaingiza Wanyarwanda wanawaambia toeni ng'ombe, mnaenda kukamata ng'ombe za Wasukuma halafu unazipiga mnada na mnada wenyewe unavyopigwa ni wa dili" alisisitiza Musukuma 

HIV/AIDS prevalence on the rise in East Africa

HIV/AIDS prevalence on the rise in East Africa
Stigmatization and discrimination among commercial sex workers, transgender, prisoners and homosexuals has been identified as the main causes for the high HIV/AIDS prevalence in East Africa.
The cases among the group popularly known as ‘key population’ are on the rise in East and Southern Africa.
This emerged during a workshop on Kenya National Advocacy convening on reducing violence and discrimination against the key population held at the Great Rift Valley Lodge in Naivasha.
According to the Vice Chair of  Kenya National Commission on Human Rights (KNCHR), George Morara, the high HIV prevalence among the group was worrying.
Addressing the press, Morara noted that HIV prevalence among the Key population was more than three times the national prevalence rates of 5.9 percent.
In terms of TB, the commissioner noted that studies had proven that the prevalence was fifty times higher in prisons in Africa.

Foreigners in S. Africa: Xenophobic Attacks a Daily Danger

Foreigners in S. Africa: Xenophobic Attacks a Daily Danger
South Africa grabbed international attention earlier this year with images of angry demonstrators attacking foreign residents and their businesses. This type of xenophobic violence, analysts say, is largely driven by high unemployment, inequality and frustration with the government’s failure to provide everyone with basic services.
But like those enduring challenges, xenophobic attacks are also proving hard to wipe out. The nation has seen eruptions of major anti-foreigner violence in 2008, 2014, 2015, 2016, and earlier this year. Members of immigrant communities and watchdog groups say xenophobic violence is a daily occurrence.
Sharon Ekambaram leads the refugee and migrant rights program for Lawyers for Human Rights. She said her rights group hears daily accounts of crimes against immigrants, and South African authorities are often reluctant to intervene when foreign nationals are targeted.

Egypt blocks 21 websites, including Al Jazeera: for “supporting terrorism”

The logo of Al Jazeera Media Network is seen during the annual MIPCOM television programme ...The logo of Al Jazeera Media Network is seen during the annual MIPCOM television programme market in Cannes, France, October 17, 2016. REUTERS/Eric Gaillard
Egypt has banned 21 websites, including the main website of Qatar-based al Jazeera television, for “supporting terrorism”, state news agency MENA and security sources said on Wednesday.
Reuters tried to access five websites named by local Egyptian newspapers and broadcasters, including the Al Jazeera website, and found them all inaccessible.
There was no immediate official comment available. An official from the National Telecom Regulatory Authority could not confirm or deny the news, but said: “So what if it is true? It should not be a problem.”

May 20, 2017

The Qatari princess, Angelina Jolie and the battle of the pyramids

Reports that Hollywood star Angeline Jolie is planning to make a movie about Sudan's history have sparked a row with Egypt, and BBC Africa's Mohanad Hashim says it is about much more than who has the biggest pyramids.
The latest twist in a long-running feud between Egyptians and Sudanese is over controversial claims that a film is to be made in Sudan to showcase the country's contribution to human civilization.
Various media have reported that a Qatari production company would fund the film, which would apparently feature Hollywood stars Angelina Jolie and Leonardo Di Caprio.
It is meant to promote historical tourism in Sudan by narrating the country's ancient Nubian history.
 The claims were so widespread that even the British ambassador to Sudan was caught up in the fray, tweeting on the story:
 Sudanese tweeters published memes showing Jolie depicted as a Nubian queen and shared reports of press conferences confirming the Hollywood star and UN ambassador would visit the country in May to scout the film's locations.

Libya death toll 'rises to 140' at Brak El-Shati airbase

Reports suggest as many as 140 people, including civilians, may have died in an attack on an airbase in Libya.
It was originally thought 60 people died when a government-allied militia tried to take over the Brak al-Shati base on Thursday.
The UN-backed government's defence minister and the commander of the militia have both been suspended pending an investigation.
The prime minister's office has denied ordering the attack.
A militia spokesman said they had "liberated the base and destroyed all the forces inside".
The town's mayor said some aircraft had been set ablaze.

May 17, 2017

DARDY'S FOOTWEAR WAUZAJI WA VIATU VYA KIJANJA DUKA LIPO MWANZA MTAA WA LUMUMBA ( DARDY'S SHOP 0762 905 207 )



















Jordan Brand to Release Air Jordan 1 Wings This Month

 





After the successful collaboration release between Just Don and Jordan Brand this past weekend, today the Jumpman announces the release date of another coveted silhouette, the Air Jordan 1 Wings. Set to release later this month, this pair of Air Jordan 1s will be limited to 19,400 pairs nationwide, with each pair of shoes numbered individually on the back of the tongue.
Dubbed as the Wings iteration, the limited edition sneakers will feature a premium leather upper in metallic gold and black. In addition, hits of black will also be featured on the midsole, shoe laces and sock liner, while an icy translucent bottom gives the sneakers a pop of blue at the bottom of each shoe.
The release of this limited edition Air Jordan 1 Wings will also tie in with Jordan Brand’s new program to inspire the youth through promoting education.
The limited edition Air Jordan 1 Wings will release this Wed., May 17, via Nike’s SNKRS draw system, with the pair retailing for a suggested price of $200.


Read More: Jordan Brand to Release Air Jordan 1 Wings - XXL | http://www.xxlmag.com/lifestyle/2017/05/jordan-brand-release-air-jordan-1-wings/?trackback=tsmclip